MANISPAA YA KINONDONI KUJENGA SHULE SITA ZA SEKONDARI
Na Jesca
Mathew
mwambawahabari
mwambawahabari
Imeelezwa
kuwa Takwimu zinaonyesha jumla ya wanafunzi 18,368 wamefaulu mtihani wa darasa
la saba katika mwaka
2015 huku wanafunzi 15,185 wakichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa chaguo la kwanza hivyo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika manispaa ya kinoondoni imesababisha wanafunzi 3,183 kukosa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2016.

Akizungumza
na Waandishi wa habari jijini Dar-es salaam mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema kuwa ili kuhakikishakwamba kila mtoto wa Kitanzania
anapata elimu bila kikwazo wilaya hiyo imeazimia kujenga shule mpya sita katika
kata ambazo hazina shule za sekondari kuanzia tarehe 5.11.2016 ili kuhakikisha
wanafunzi wote waliofaulu wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Aidha
ameongeza kuwa lengo la zoezi hilo ni
kukamilisha shule za kata katika kata 6 ambazo ni tandale,mzimuni ,ubungo,kimara,kinondoni,magomenina
mbezi juu ndani ya miezi 2 ili kuwawezesha vijana 3183 upata nafasi ya kujiunga
na masomo ya sekondari.
Post a Comment