WAZIRI WA MAGUFULI ATUMBUA MAJIPU : AIFUNGIA KAMPUNI YA SIMU,PIA AZIFUNGIA REDIO 28 NCHINI,SOMAZAID
Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Masiliona,Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa |
Mwamba wa
habariblog
SERIKALI nchini imetangaza kuifungia kampuni ya simu ya six
Telecom pamoja na kuifungulia jarada la kiuchunguzi polisi, baada kubainika kuwa
ilikosesha serikali mapato yaliyotokana na kodi yanayofikia bilioni 8.5 pamoja
na kutoza gharama ya simu kwa wateja kwa kiwango cha
chini tofauti na ile iliyopangwa na serikali.
Hata hivyo,Serikali pia imetangaza
kuzifungia redio 28 nchini baada ya kushindwa kulipia ada ya Leseni.
Akitangaza uaamuzi huo,leo jijini Dar es
Salaam wakati wa mkutano na waandishi,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imefikia uamuzi
wa kuifungia Kampuni hiyo ya simu baada ya kufanya makosa mbali
mbali,
Waziri Mbarawa ameyataja makosa hayo
kuwa ni kuikosesha mapato serikali yaliofikia billion 7.2 na kukataa
kulipa ada ya reseni ambayo ni bilioni 1,pamoja na kugoma kulipa toza ya faini
ya milioni 361.25
“Kwaanzia sasa tumeifungia kampuni hii ya Six
Telecom baada ya kukiuka sheria mbalimbali ambapo Kampuni hii ya simu
ilisajiliwa kutoa huduma mwaka 2013,lakini ikaanza kukiuka kanuni za
Mamlaka ya mawasilioni nchini (TCRA) ambayo iliweka kiwango cha chini cha
gharama kwa kupiga simu nje ya nchi wakati ilitakiwa kutoza gharama kubwa,”
“Licha kutoza kiwango hiki cha chini
ya kiwango pia imeshindwa kulipa kodi ya Bilioni
7.2 pamoja na kukataa kulipa gharama za reseni inayofikia
bilioni 1 na kushindwa kulipa faini ya milioni 361.25 iliyotokana
kukiuka kanuni za huduma hiyo”amesema Mbarawa.
Vilevile,Waziri Mbarawa ametangaza kuzifungia
rasmi redio 28 nchini baada ya kushindwa kulipa ada ya reseni kwenye
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA jambo analodai kuwa ni kosa.
“Tumezifungia redio 28
ambazo Kesho (TCRA) watazitaja kwa majina,kwani redio hizi zimeshindwa kulipa
ada ya reseni ambapo kisheria wanatakiwa kulipa,lakini redio hizi zilishindwa
kulipa ”amesema Waziri Mbarawa
Post a Comment