JESHI LA POLISI MKOANI PWANI LAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUKESHA KWENYE VILABU VYA POMBE WANACHOCHEA UHARIFU
NA VICTOR MASANGU, PWANI
mwambawahabari
KATIKA kukabiliana na wimbi la uharifu Jeshi
la Polisi Mkoa wa Pwani limepiga marufuku kwa watu wenye tabia ya kukesha
katika vilabu vya pombe usiku kucha, na kucheza pool kuanzia asubuhi mpaka
usiku wa manene ,hali ambayo ndio imekuwa ikichangia kwa kiasi
kikubwa kuwepo kwa vitendo vya wizi, unyang’anyi pamoja na ujambazi.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake kuhusiana na mikakati waliyojiwekea katika kupambana na
uharifu Kamanda wa Polis Mkoa wa Pwani kamishina msaidizi Boniventura Mushongi
amesema kwamba kwa sasa wameanza kufanya msako mkali katika maeneo ya Mkoa wa
Pwani ya kuwasaka watu ambao wanajihusiha na vitendo vya ujambazi.
Kamanda Mushongi alisema
kwamba tabia ya baadhi ya watu kukesha katika maeneo hayo
ya vilabu vya pombe wamebaini wanajihusisha na uchezaji
wa kamali, uuzaji wa bangi hivyo kupelekea kufanya matukio ya uporaji wa
mali za watu katika nyakati hizo za usiku kwa wapiti njia na wale ambao
wamekwisha pumzika majumbani kwao
“Jamani waandishi kwa sasa sisi kama jeshi la
polisi Mkoa wa Pwani tumejipanga vilivyo na tutafanya msako katika maeneo mbali
mbali yote hii ni kuhakikisha wimbi la uharifu linapungua na kwa sasa hatutaki
kuona watu wanakesha baa kwani wao ndio chanzo vha kusababbisha kutokea kwa
uharifu,”
“Maana kuna baadhi ya watu wanakesha katika
vilabu vya pombe kumbe wengine wanavuta muda wa usiku ndipo waanza kufanya
matukio yao ya uharifu kwa hiyo hatutakio kuona mtu yoyote anashinda katika
vilabu hivyo sambamba na kucheza pool kuanzia asubuhi mpaka saa nane za siku ni
marufuku kwanza ni kinyume cha sheria na taratibu ,”alisema Kamanda.
Aidha Kamanda huyo aliwataka wananchi wa Mkoa
wa Pwani kwa kushirikiana na wazazi kkuachana na uwogo na badala yake sasa
wahakikishe wanashirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu bila
ya kuwa na uwoga wowote na pindi watakapoona wana mashaka na mtu watoe taarifa
katika vyombo husika.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo
alibainisha, sababu nyingine zinazochangia kwa kisi kikubwa kutokea
kwa wimbi la uharifu ni kutokana na baadhi ya watu kunywa ombe
kupita kiasi pamoja na madereva wa pikipiki kushirikiana na waharifu katika
kufanya matukio hayo ya uporaji.
Kufuatia kaluli hiyo iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Tanzania daima iliweza kuzungumza na baadhi ya
madereva wa pikipiki akiwemo Hussen Ally pamoja na Nassoro Bala ambao walisema
kwamba kuna baadhi ya madereva wa pikipiki wanavunja sheri kwa
makusudi ikiwemo kunywa pombe wakati wanaendesha chombo cha moto.
Walisema kwamba wakati mwingine matukio ya
uharifu yanajitokeza bila ya wao kujua kwani wakati mwingine wanaweza kupakia
abiria zaidi ya mmoja kumbe wote waliopanda ni waharifu na matokeo yake
wanapofika njiani wanaipora pikipiki hiyo na kumjeruhi dereva au wakati
mwingine wanaamua kumuuwa.
Hata hivyo uchunguzi uliofanyuwa na Mwandishi
wa habari hizi uliweza kubaini katika Mkoa wa Pwani kwa sasa bado
unakabiliwa na wimbi la uharifu kutokana na baadhi ya vijana wengi wa mitaani
kutokuwa na kazi hivyo kujiingiza katika uharifu hali ambayo imekuwa ni tishio
sana kwa wananchi hasa katika eneo la maili moja , lililopo Wilaya
ya Kibaha, pamoja na eneo la Kiluvya lililopo Wilaya ya Kisarawe
hivyo kuhahitajika juhudi za makusudi kwa jeshi la polisi
kukabiliana na hali hii.
Post a Comment