JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LAENDESHA OPERESHENI KUNASA MAJAMBAZI
kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro akionesha silaha walizo kamata kutoka kwa majambazi
na John Luhende
na John Luhende
mwambawahabariblog
JESHI la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limesema linaendesha operesheni kali ili kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali jijini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari kamamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Simoni Sirro amesema opereshenihiyo itahusisha ukamataji majambazi wa wanaopora kwa kutumia pikipiki na waharifu wengine
na amewatahadharisha wananchi kutobeba kiasi kikubwa cha fedha kutoka benki bila kuwa na ulinzi kutoka katika jeshi hilo.
“kuna namna nyingi za kuhamisha fedha zikiwemo za kutumia mitandao ya simu,ni vizuri kutumia njia hizo kuliko kubeba fedha mkononi bila ulinzi”alisema Sirro.
Aidha, Kamishna Sirro amesema jeshi hilo limekamata majambazi na silaha mbaimbali ikwemo bastola zilizo kuwazikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu
Pia ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za waalifu ili kuondoa wimbi la uhalifu linaloendelea kushamiri siku hadi siku.
Post a Comment