Ads

TALGWU YATOA TAMKO NA KULAANI MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YABAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI


Na John Luhende 
mwambawahabari
Chama cha wafanyakazi  wa serikali za mitaa  TALGWU  kimelaan  matumizi mabaya ya madaraka yanayo fanywa na baadhi ya viongozi wa serikali dhidi ya watumishi wake  kwa kuitafsiri vibaya kauli mbiu ya Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Dk John  Magufuli  ya hapakazitu kwa kuwanyima likizo  na kuwa weka ndani baadhi ya watumishi  kana kwamba   wamefanya   makosa  ya jinai  kinyume cha sharia.

Akizungumza na waandishi wa habari  kny katibu mkuu wa wa TALGWU Kibwana   Njaa amesema   baadhi ya  unyanyasaji  na  matumizi mabaya yaliyo fanywa nipamoja na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kuwa weka ndani  muda wa masaa sita,  maafisa ardhi  Zaidi ya kumi  kutokana na kuchelewa kufika eneo la mkutano kusikiliza migogoro ya ardhi,  wafanyakazi kusimamishwa kazi kupitia vyombo vya habari na mbaya Zaidi viongozi wanao toa  hukumu hizo si mamlaka ya nidhamu ya watumishi  mfano katibu tawala wa mkoa wa Kigoma  John Ndunguru aliwasimamisha kazi watumishi sita wa halma shauri ya ujiji  wakati ofisi ya mkoa siyo mamlaka ya nidhamu ya watumishi hao.

Amesema matukio hayo  na mengine yanayo fanana na hayo yanaonesha wazi kwamba   baadhi ya vingozi wa serikali  kwa kuelewa ama   kwa kuto elewa wanatumia vibaya falsafa ya hapakazitu.

“Swali la kujiuliza ni, je uchunguzi ukikamilika  na ikabainika watumishi hao walionewa  Serikali itatumia vyombo vya habari kusafisha majina yao? Natakaieleweke kuwa TLGWU haiwatetei wafanyakazi ambao wanaenda kinyume nasheria ,kanuni  na taratibu za kazi  lakini  tunataka taratibu zifuatwe  na hatimaye watumishi wachukuliwe hatua stahiki

Hatahivyo  alieeza kuwa wafanyakazi wanaidai serikali mabilion ya pesa  lakini  wao hatasiku moja hawajawahi kuidhalilisha kama wanavyo fanya baadhi ya viongozi hawa kama chama wamendelea kuwa wavumilivu  na wamejikita kufufuata taratibu  ikiwa pamoja na kufanya majadiliano  ya  mara kwa mara na serikali  kuhusu deni la blioni 18 kwa heshima.

 Aliweka wazi pia tabia ya  ya baadhi ya viongozi hasa wakuu wa mikoa na Wilaya kutoa maagizo ya kusitisha likizo  kinyume  cha utaratibu , ambapo imejitokeza katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kuzuia likizo za watumishi mwishoni mwa mwaka 2015 ,likizo ni haki ya mtumishi kwa mujibu wa sharia ambapo mtumishi anapaswa kupata likizo mara moja kwa mwaka ingawa kila Halmashauri ina utaratibu wake na ratibazake za likizo kwa watumishi wake.

“sasa unaposimamisha kundi kubwa la wafanya kazi wasiende likizo maanayake una vuruga utaratibu  mzima wa  wa likizo kwa Halmashauri hiyo’’


Chama kina kinampongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na ufisadi  pamoja na rushwa  na wana  amini kuwa  uchumi wa nchi utakuwa na manufaa kwa wafanyakazi na maslahi yao yataboreshwa Pamoja na hayo ametoa wito kwa vingozi wa kisiasa  watambue wajibu wao nadhamana  kubwa waliyopewa  na Taifa na watumie mamlaka  yao kwa mujibu wa sharia ,kanuni na taratibu za nchi, vinginevyo chama hakita sita kuwafikisha Mahakamani viongozi wa aina hiyo kwa ukiukaji wa  sharia za Nchi.





No comments