Ads

CCM YA SEMA UCHAGUZI LAZIMA URUDIWE ZANZIBAR



MUDA mchache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) 

Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kasoro na athari za kurudia 

Uchaguzi uliofutwa kinyume cha sheria na Jecha Salim Jecha, 

viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametangaza kuwa 

uchaguzi  huo lazima urudiwe.


Wakizungumza jana na vijana wa chama cha Mapinduzi katika 

viwanja vya Maisara waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya 

matembezi ya kuunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar,viongozi wa juu 

wa chama hicho walisisitiza kuwa uchaguzi wa Zanzibar upo pale 

pale na utarudiwa kadiri tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) 

itakavyotangaza.

Wa kwanza kutoa msimamo huo alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais, 

Balozi Seif Ali Iddi, aliyesema kuwa uchaguzi huo utarudiwa hata 

ikiwezekana vyama vyote vikijitoa CCM kitashiriki peke yake

“Uchaguzi wa marudio upo pale pale, tunajua uchaguzi ulifutwa 

kihalali, mjitayarishe kwa uchaguzi wa marudio. CUF wamesema 


watatumia nguvu ya umma, tunawakaribisha na wataona matokeo 

yake” alisema Balozi Iddi.

Katika mkutano huo uliokuwa unarushwa moja kwa moja na kituo 

cha Televisheni cha ZBC, Dk  Alli Mohamed Shein alipongeza 


msimamo wa Balozi Iddi, na kusema atabaki kuwa rais hadi 

uchaguzi utakaporudiwa.

Dk Shein alisema yupo madarakani kwa kushauriwa na 

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwamba hajavunja katiba na kama 

itatokea mahakama ikatoa ufafanuzi kuwa anakosea kuwepo hapo 

kikatiba basi ataondoka madarakani


“Mahakama ikisema nakosea nitaondoka, Rais yupo Baraza la 

Mapinduzi lipo na Mawaziri wapo, nitaita waandishi wa habari Ikulu 

na mimi nimjibu Maalim Seif kwani kuna mengi 

amenisingizia” alisema.

No comments