Ads

BODI YA MIKOPO YATOA MABILION KWA WANAFUNZI

Na Jesca Mathew.
mwambawahabariblog
Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imetoa jumla ya tsh  bilioni 459 kwa wanafunzi wa elimu ya juu 122,486 wanaosoma katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi katika mwaka wa masomo 2015/2016.
Hayo yameelezwa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano Omega Ngole amesema kuwa hiyo ni idadi kubwa ya wanafunzi walionufaika na mkopo huo tangu kuanzishwa kwa bodi mwezi julai 2005.

"Katika mwaka uliopita wa masomo 2014/2015 serikali kupitia bodi ilitoa jumla ya tsh bilioni 341 ziliwanufaisha wanafunzi 99,069 alisema".

Kati ya fedha zilizotolewa jumla ya tsh bilioni 199.7 zilikwenda kwa wanafunzi wa masomo ya mwaka wa kwanza 53,537 na tsh 259.1 bilioni zililipwa kwa wanafunzi 68,916 wanaoendelea na masomo wa mwaka wa pili na kuendelea katika vyuo vya umma na binafsi.

Bwana omega ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya bdi ya mikopo  iliyotolewa kundi kubwa la wanafunzi wanaopata mikopo ni wale wanaosoma program za kipaumbele ambazo ni udaktari wa binadamu,udaktari wa meno,udaktari wa wanyama,ufamasia na uuguzi na ualimu wa masomo ya sayansi na hesabu pamoja na yatima na walemavu.

Hata hivyo bodi ya mikopo inatoa wito kwa waajiri katika taasisi za uma na binafsi nchni kuhakikisha wanazingatia sheria liyoanzishwa na bodi hiyo inayowataka kutambua waajiriwa ambao ni wanufaika wa mikopo inayotolewa na bodi ili kukata sehemu ya mishahara na kuiwasilisha kwa bodi kama marejesho.


Ikumbukwe kuwa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria no.9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi mwezi juai 2005 ikiwa na majukumu ya kutoa mikopo kwa wanafunzi pamoja na kusimama urejeshi wa mikopo kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo.  

No comments