Na Magreth Kinabo
mwambawahabariblogspot.com
Serikali imenunua
mashine mpya ya CT-Scan yenye thamani ya takriban dola za
Marekani milioni 1.7 yenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili
ya kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili(MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Ununuzi wa mashine
hiyo, umefanyika kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoifanya hivi karibuni ambapo
aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma zake na kuhakikisha vifaa
tiba na dawa vinapatikana ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma
bora za afya.
Hayo yamegundulika
leo baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangala aliyoifanya leo katika hospitali
hiyo, ambapo alitembea Idara ya Magonjwa ya Dharura,Idara ya Mionzi, sehemu mpya
ya wagonjwa waliopo chini ya ungalizi maalum(ICU), ambayo inafanyiwa ukarabati
na wodi mojawapo.
Naibu Waziri
akitembelea katika Idara ya Mionzi ambapo alijionea mashine za MRI
na CT –Scan zinavyofanyakazi.
Akizungumzia
kuhusu mashine ya CT-Scan Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dkt. Flora Lwakatare alisema
mashine hiyo , iliyotengenezwa na kampuni ya Siemens mpya
imefungwa siku mbili zilizopita na imeshaanza kufanya majaribio kwa
wagonjwa 26 tangu ilipofungwa
Dkt. Flora
aliongeza kwamba mashine hiyo iko moja tu nchini na katika nchi za Afrika
Mashariki nchi nyingine iliyonunua mashine hiyo ni Kenya katika Hospitali ya
Aghakhan.
“ Mashine hii inatoa
huduma za hali ya juu kwa magonjwa ya moyo, ubongo tumbo kifua na inauwezo wa
kupima kifua na tumbo kwa sekunde sita,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu mashine hiyo Naibu Waziri huyo, alisema imenunuliwa kwa fedha za
Serikali wala sio mkopo.
“Tunatarajia kununua
mashine hii katika hospitali ya Dodoma na Mwanza,” alisema Waziri Kingwangala.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa MNH, Profesa Laurence Maseru alisema mashine
hiyo ina sahani 128 mara 2 ikilinganishwa na iliyokuwepo ambayo ilikuwa
inatumia sahani sita.
Kwa upande wa
mashine ya MRI ambayo tangu ilipofanyiwa matengenezo makubwa Novemba 26, mwaka
jana hadi sasa imesha hudumia wagonjwa 560.
Dkt.
Kingwangala alitembea katika Idara cha huduma za dharura
na kuangalia jinsi huduma zinavyotolewa, ambapo alielezwa na Mkuu wa Idara
ya Magonjwa ya Dharura Dkt. Juma Mfinaga alisema ambayo huhudumia wastani wa
wagonjwa 300 hadi 400 kwa siku ambacho kinafanya kazi kwa kutumia mfumo maalum
wa kompyuta bila kutumia karatasi.
Naibu Waziri huyo,
mbali na kupongeza maboresho yaliyofanyika na huduma nzuri, alitoa maagizo kwa
uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma za zilinazotolewa
hospitalini kuwa za kitaifa zaidi.
Alitolea mfano huduma
kulipa kwa kuongeza vitanda na matumizi ya choo kimoja kila chumba ili kuweza
kuvutia wateja.
“Sisi tunaweza
kufanya biashara kwa kuboresha huduma za kulipa ili zimpendeze na kuvutia
wateja. Na fedha zitakazopatikana zitatumika kununua dawa , vifaa tiba na
kuwapatia wafanyakazi motisha, alisema.
Aliutaka uongozi huo pia
kuhakikisha inawalipa wafanyakazi fedha za malipo ya ziada kwa
wakati ifikapo tarehe 25 ya mwezi unaofuata,kutumia mfumo wa kompyuta sehemu
zote, kupunguza msongamno wa wagonjwa na kuwa wabunifu.
Post a Comment