Mahakama ya Ardhi yaweka zuio la bomoa bomoa Wilaya ya Kinondoni
Mwambawahabariblogspot.com
picha na maktaba
Na Raymond
Mushumbusi
Mwambawahabariblogspot.com
Mahakama Kuu ya Tanzania
Kitengo cha Ardhi imeweka zuio la kubomoa nyumba zilizopo katika wilaya ya
Kinondoni hasa zile ambazo wamiliki wameleta ombi lao mahakamani kuzuia
kubomolewa.
Akitoa hukumu hiyo mbele
ya walalamikaji Mwanasheria wa Serikali, mawakili wa walalamikaji na wananchi
Jaji wa Mahakama hiyo kuu ya Ardhi Mhe.Panterine Kente amesema kuwa mahakama
imezingatia maelezo toka pande zote mbili na kuangalia madhara watakayopata
wananchi kwa kutekelezwa kwa zoezi hilo.
Jaji Panterine Kente
ameongeza kuwa mahama ya Ardhi haijaweka zuio la bomoa bomoa kwa Tanzania nzima
bali kwa wale tu walioleta maombi ya shauri la zuio la kubomolewa nyumba zao na
kusisitiza kuwa Serikali itaendelea na uwekaji wa alama za x na
ubomoaji wa nyumba zilizopo sehemu hatarishi na sehemu zisizostahili.
“ Nakuagiza Wakili
Abubakari Salim uniletee majina yote leo hii na sio kesho ya waliofungua shauri
la zuio la kutobomolewa nyumba zao ili tuweze kuendelea na zoezi la ubomoaji”
Alisema Jaji Kente
Akizungumza baada ya
kutolewa hukumu hiyo Wakili wa Serikali Manchare Henche amesema wamepokea
hukumu hiyo na wao wataendelea na majukumu yao ya ubomoaji wa meneo hatarishi
kama Mahakama ilivyoeleza kuwa haijatoa zuio la bomo bomoa kwa Tanzania nzima
ila kwa wale tu walioleta shauri la zuio.
“Tunaomba walio maeneo
ya mabondeni wahame kwani zoezi hili linaendela na zoezi la uwekaji wa alama za
x litaendelea kama kawaida kwa maeneo mengine nje ya haya yaliyowekewa zuio”
Alisema Subuta.
Aidha akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kutolewa hukumu hiyo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni
Maulid Mtulia amesema kuwa uamuzi umeridhisha na pia mahakama imetenda haki kwa
wananchi wa kinondoni na wanashukuru kwa kupata nafasi ya kusikilizwa kwa hoja
zao.
Kesi hiyo namba
822ilifunguliwa na wawakilishi wanane wanaowawakilisha wanachi 674
ambao nyumba zao zilikuwa katika mpango wa kubomolewa chini ya
sheria za mipango miji.
Baada ya Mahakama kuu ya
Tanzania kitengo cha Ardhi kutoa zuio la bomoa bomoa kwa wakazi hao kesi ya
msingi itatajwa tena januari 11.
Mwambawahabariblogspot.com
Post a Comment