Serikali yataka halmashauri kutenga bajeti ya damu
Na Magreth Kinabo
mwambawahabariblog
Serikali imezitaka kila
halimashauri nchini kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya
damu ili kuwezesha wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kuipata na kuepusha
kupoteza maisha ya watu hususan wakina mamawajazwazito na watu waliathirika na
ajali.
Aidha Serikali imesema
damu hutolewa bure, hivyo mtu yoyote atakayeuziwa damu ataoe taarifa
kwa mkuu wa wialaya , mkuu wa mkoa au wizarani ili wahusika waeze
kuchukuliwa hatua. Hivyo Watanzania wasikubali kutoa rushwa kwa ajili ya kupata damu.
Kauli hiyo imetolewa leo
na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangala aliyoifanya leo katika Ofisi za
Mpango wa Taifa wa Damu zilizopo jijini Dares Salaam.
Awali akitembelea ofisi
hizo, Dkt Kingwangala alielezwa na Dkt . Avelina Mgasa kwamba
changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga
bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo.
“ Mganga Mkuu au
Mkurugenzi ambaye ahatawajika kukaikisha damu inakuwepo katika vituo vya
kutolea huduma ataripotiwa kwa mmlaka zilizomteua ili ziweze kumchukulia
hatua,” alisema Dkt. Kingwangala.
Dkt. Kingwangala
aliitaka mifumo ya bima nchini kuhakikisha iligharamia mifuko ya kuhifadhi damu
na reagent(vitenganishi) kwa wagonjwa waowalipia huduma za afya ili
kuweza kusiadi changamoto inayoikabili ofisi hiyo.
Post a Comment