JK AMPONGEZA SAMATA KWA KUTWAA TUZO
Na Raymond Mushumbusi
mwambawahabariblog
Rais mstaafu wa Awamu ya
Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Nahodha wa Timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta kwa kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora
Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani Afrika kwa mwaka 2016.
Pongezi hizo amezitoa
leo Jijini Dar es salaam alipokuta na Naodha huyo katika Ofisi za Chama Cha
Mapinduzi (CCM) zilizopo Lumumba Jijini Dar es salaam.
Dkt.Kikwete alimpongeza
Nahodha huyo (Mbwana Samatta) na kumtaka kuongeza juhudi zaidi ili aweze
kucheza katka Ligi kubwa Barani Ulaya.
“Natamani siku moja tuwe
tunakuangalia Samatta ukifunga magoli katika Ligi kubwa Barani Ulaya kama vile
Ligi kuu ya Uingereza” Alisema Dkt Kikwete.
Kwa upande wake, Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa Wizara
imepata faraja kubwa kwa Samatta kuiwakilisha Tanzania katika tuzo hizo za
Kimataifa kwa kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho.
Aidha, Mbwana Samatta
alisema kuwa, anamshukuru Rais mstaafu Mhe. Dkt. Kikwete kwa kumpa moyo wa kupambana
na ameishukuru pia Serikali ya Awamu ya tano kwa kumuunga mkono katika
kupeperusha bendera ya taifa katika soka la kimataifa.
Samatta aliibuka kuwa
Mchezaji Bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika baada ya
kuwabwaga wenzake wawili kwenye kinyang’anyiro hicho, akiwemo mchezaji mwenzake
wa TP Mazembe,Kipa Robert Kidiaba pamoja na Mualgeria,Baghdad Boundjah
anayeichezea Klabu ya Etoile Du Sahel ya nchini Algeria.
Post a Comment