Ads

WANACHI WASHAURIWA KUTUMIA KITUO CHA KURATIBU MATUKIO YA SUMU


MratibuwaKituo cha kuratibumatukio ya sumunchinitokaOfisi ya MkemiaMkuuwaSerikali Bw. YohanaGoshashyakiwaelezawaandishiwahabarileoJijini Dar es salaam kuhusuumuhimuwakituohichohapanchiniikiwemokuwakinga na madhara ya sumukwakutoaelimujuu ya matumizisahihi ya kemikalimbalimbali.kushotoniAfisaHabariwaIdara ya HabariMaelezo Bw. Frank Mvungi.picha na  (Benedicta Liwenga)

Na Jovina Bujulu 
mwambawahabariblog

Serikali imewataka wananchi kutumia kituo cha kuratibu matukio ya sumu wapatapo madhara yatokanayo na Sumu kote nchini.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kituo hicho kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali  Bw. Yohana Goshashy wakati wa mkutano na Vyombo vya habari leo Jijini Dar es salaam.

“kwa sasa matukio mengi yanayotolewataarifa kituoni hapo ni dawa za kulevywa na dawa za kuulia wadudu waharibifu kwenye mimea(viuatilifu)” Alisema Ndudu Goshashy.

Akizungumzia majukumu ya kituo hicho Ndugu Goshashy alisema kuwa ni pamoja na kutoa taarifa za matukio ya sumu, kuzuia ajali za kemikali na kuratibu matukio ya Sumu, uchunguzi na utambuzi wa sumu mbalimbali na kufanyatafiti mbalimbali zinazohusiana na kemikali na sumu.

Aidha Ndugu Goshashy alisema kuwa kituo hicho kina wajibu wa kuzitahadharisha mamlaka husika juu ya uwepo wa viashiria vya athari za sumu ili hayua stahiki ziweze kuchukuliwa kuzui athari hizo.

“Taarida za tahadharizinaweza kusaidia kuweka mfumo wa udhibiti na usimamiaji wa kemikali na sumu kuweka alama ya utambulisho au kuiondoa bidhaa sokoni” alisema Ndugu Goshashy.

Akizungumiza utoaji waelimu kwa umma kuhusu huduma zitolewazo na kituo hicho Ndugu Goshashy alisema kwamba wanaelimisha kuputia vyombo vya habari, kutoa namba za simu na kuchapisha vipeperushi na kuisambaza.

“Tunatoa ushauri kuhusiana na dawa za kulevya, jinsi ya kuyaepuka na kushauri aina sahihi za vifumbua sumu” aliongeza Ndugu Goshashy.

Aidha ndugu Goshashy aliwashauri wananchi kuepuka madhara yanayoweza kutokea na kutoa taarifa za matukio mbalimbali kama kula, kunywa au kuvut.

No comments