Ads

TBS YATEKETEZA TANI 39 ZA BIDHAA ZA CHAKULA ZISIZOKIDHI VIWANGO








Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeteketeza tani 39 za bidhaa za chakulazisizokidhi matakwa ya viwango, zenye thamani ya takribani Sh milioni 149.


Zoezi hilo limefanyika leo, Agosti 17, 2026, Mbezi Gongoni, Wilaya ya Mkuranga, Pwani, baada ya bidhaa hizo kubainika kupitia ukaguzi uliofanyika katika kipindi cha Julai hadi Agosti.


Kwa mujibu wa TBS, baadhi ya bidhaa hizo, Hazikuwa na alama ya ubora, Zilikosa maelezo sahihi kwenye vifungashio, zilikuwa hazina taarifa kwa Kiswahili au Kiingereza kama inavyotakiwa na baadhi zilikuwa zimekwisha muda wa matuzi


TBS imewasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha bidhaa wanazoingiza au kuuza zinakidhi viwango vilivyowekwa, huku wananchi wakihimizwa kusoma maelezo ya bidhaa na kuangalia alama ya ubora kabla ya kununua au kutumia.


Hatua hii ni sehemu ya juhudi za TBS kulinda afya za wananchi na kuhakikisha bidhaa salama na zenye ubora zinafika kwa watumiaji.

No comments