RC CHALAMILA AJIONEA UKIUKWAJI WA SHERIA PARKING ZA MAROLY, ATOA GIZO KWA WILAYA YA TEMEKE KUUNDA KIKOSI KAZI
-Akagua maeneo ya maegesho ya malori yasiyo rasmi Temeke asema uholela Dar hauvumiliki.
-Afika katika daraja linaunganisha wananchi wa kata ya Toangoma na Kata ya kibondemaji aelekeza TARURA kufanya tathimini ili kuja na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa daraja la kudumu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke na RPC Temeke kuunda kikosi kazi maalumu cha kukamata madereva wa malori wanaoegesha kwenye maeneo yasiyorasmi hususani hifadhi za barabara ambapo ameagiza madereva wote wanaopaki kwenye hifadhi za barabara wakamatwe na kuhojiwa kwa hatua zaidi.
RC Chalamila ameyasema hayo leo Agosti 17, 2026 Wilaya ya Temeke Jijini humo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo barabara ya mandela na kata ya Sandali na kujionea malori mengi yakiwa yamepaki kwenye hifadhi za barabara na mengine kuziba barabara kinyume na maelekezo aliyowahi kuyatoa hivi karibuni, hivyo ametangaza rasmi kuanza kukamatwa madereva wasiozingatia maagizo hayo.
Aidha RC Chalamila ametumia ziara hiyo kurejea maagizo yake ya kutaka wamiliki wa bandari kavu kuhakikisha wanakuwa na maegesho ya malori ndani ya maeneo yao ili wasiegeshe kwenye hifadhi za barabara na wasizibe barabara na kuzuia watumiaji wengine wa barabara huku akimtaka mkuu wa wilaya ya Temeke kuwaita kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wamiliki wa bandari kavu siku ya jumatano agosti 19 ili awapatie maelekezo zaidi
Sanjari na hayo RC Chalamila alikwenda kukagua daraja linalouunganisha Kata ya Toangoma na Kata ya Kibondemaji, hususan Mtaa wa Golani B na Mtaa wa Kichangani ambapo amejionea daraja lililojengwa miaka michache iliyopita na wananchi kwa nguvu zao wenyewe, lakini halina ubora unaohitajika hivyo ameagiza TARURA mapema iwezekanavyo kufanya tathimini na kuja na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa daraja la kudumu katika eneo hilo ili kuondoa kero ya muda mrefu inayowakabili wananchi hao.
Vilevile kupitia ziara hiyo
ameweka msisitizo kwa mabasi yote ya mikoani na nchi jirani kurejea kupaki kwenye kituo cha mabasi cha Magufuli badala ya kuendelea kuegesha eneo la Shekilango na maeneo mengine yasio rasmi ikiwa ni katika mkakati wa kumaliza msongamano wa magari katika Mkoa huo.
Katika ziara hiyo wananchi wa kata ya Sandari pamoja na madereva wa malori wameeleza changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maegesho ya malori, uharibifu wa mazingira kutokana na Salfa inayotoka bandari kavu eneo la sandari pamoja na ukosefu wa barabara za ndani ya kata ya sandali .
Hata hivyo Mkurgenzi wa Halmashairi ya Manispaa ya Temeke Ndg Jomari Mrisho Satura amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa kilio hicho cha wananchi na maelekezo yote yaliyotolewa yanakwenda kufanyiwa kazi
Post a Comment