Ads

Zogo Mchongo Msimu wa nne wazinduliwa rasmi

  





Na Fancisco Peter


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amezindua rasmi msimu wa nne wa Zogo Mchongo, kipindi cha Benki ya CRDB kinachotoa elimu ya fedha kwa jamii. 



Mchongo huo umezinduliwa leo  Jumatano ya tarehe 22, Julai kwenye Ofisi za makao makuu ya Benki ya CRDB, Palm Beach, Dar es Salaam 


Akizungumza katika hatua za uzinduzi huo Makonda   ameainisha kuwa CRDB ni mfano wa kuigwa maana imeendelaza jitihada za sio tu kuwa Benki bali ni sehemu ya mafunzo kwa jamii katika masuala ya kifedha.


Zogo Mchongo msimu wa nne imekuja kiutofauti ikiwa kidijitali zaidi huku ikishirikisha maswali ya mtandaoni pamoja na zawadi kemkem.


Benki ya CRDB imeongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Abdulmajid Nsekela, Afisa Mkuu wa Biashara, Boma Raballa, Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Bi. Joseline Kamuhanda, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Bi. Yolanda Uriyo , mameneja wa kanda na wafanyakazi wengine wa Benki.


“𝐍𝐢 𝐁𝐞𝐧𝐤𝐢 𝐲𝐚 𝐂𝐑𝐃𝐁 𝐩𝐞𝐤𝐞𝐞 𝐲𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐦𝐚𝐮𝐝𝐡𝐮𝐢 𝐲𝐚𝐧𝐚𝐲𝐨𝐭𝐨 𝐞𝐥𝐢𝐦𝐮 𝐲𝐚 𝐟𝐞𝐝𝐡𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐣𝐚𝐦𝐢𝐢, 𝐧𝐚 𝐤𝐢𝐩𝐢𝐧𝐝𝐢 𝐜𝐡𝐞𝐧𝐲𝐞𝐰𝐞 𝐧𝐢 𝐙𝐨𝐠𝐨 𝐌𝐜𝐡𝐨𝐧𝐠𝐨, 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐲𝐨 𝐦𝐬𝐢𝐦𝐮 𝐰𝐚𝐤𝐞 𝐰𝐚 𝐧𝐧𝐞 𝐮𝐧𝐚𝐳𝐢𝐧𝐝𝐮𝐥𝐢𝐰𝐚 𝐥𝐞𝐨”amesema Dkt  Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya CRDB.

No comments