MUHIMBILI YADHIMISHA SIKU YA UGONJWA WA HOMA YA INI KWA KUTOA HUDUMA YA KUPIMA BURE
Mwamba wa habari
Daktari Bingwa mbobezi wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Swaleh Pazi, amesema ugonjwa wa homa ya ini aina ya virusi B unaweza kuambukizwa kwa njia mbalimbali, ikiwemo mtoto kuzaliwa akiwa na maambukizi kutoka kwa mama mwenye virusi hivyo.
Amesema njia nyingine za maambukizi ni kuongezewa damu isiyo salama, kutumia vifaa vyenye ncha kali kwa kushirikiana pamoja na matumizi ya sindano kwa watu wanaotumia dawa za kulevya.
Aidha amesema kunawagonjwa wa homa ya Ini zaidi ya 5,000 wanahudhuria clinic katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Daktari bingwa huyo ameeleza hayo alipozungumza na waandishi wa habari katika Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani inayofanyika kila mwaka Julai 28, ikiwa na lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu kinga, uchunguzi wa mapema na matibabu ya ugonjwa hu.
Hospitali ya Taifa Muhimbili imeadhimisha sikuhiyo katika kituo chake kilichopo stesheni jijini Dar es salaam Kwa kutoa huduma bure kupima maambukizi ya homa ya Ini

Post a Comment