Ads

MH PAUL MAKONDA: NIMEMUOMBA RIO FERDINAND ASIPOST KAMA YUPO TANZANIA




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema amemuomba Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza Rio Ferdinand, asichapishe ‘Ku-Post’ kwa sasa kuwa yupo Tanzania, akieleza kuwa hilo sio jambo muhimu ikilinganishwa na kazi aliyo nayo ya kuinua vipaji vya Vijana wa Kitanzania.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 22, 20206, Jijini Dar es salaam, Makonda amesema kumekuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya Kijamii kuhusu kwa nini Rio ‘Hajapost’ kuhusu ujio wake Nchini, badala ya kuangalia Ajenda Kuu ya Maendeleo.


“Wakati mwingine tunapenda kubeza mambo lakini hatujui nguvu kubwa inayofanywa na Viongozi wetu kufanikisha hayo mambo, ajenda kubwa ilikuwa ni kwanini Rio hajapost kwenye Akaunti yake kuwa yupo Tanzania na Watu wakawa wanamfuatilia kuona ataweka post gani ili waamini yupo Tanzania.” Amesema Makonda


Aidha, ameongeza kuwa mara nyingi Watu hujikita kwenye Mitandao ya Kijamii badala ya kuangalia manufaa ya muda mrefu yanayoweza kupatikana kupitia ushirikiano kama huo.


“Tunapenda kujadili mambo kwa kuyaona bila kuyajua na mwisho tunaamini tunajua kila kitu, ulishawahi kufikiria Mtu yupo na anaongelea mema juu ya Nchi yako, namna Serikali inavyopiga hatua, halafu wewe badala ya kuchukua ile content uipeleke Duniani unataka yeye ndio apost?” Waziri Makonda.

No comments