KAMATI YA BUNGE YAJENGEWA UWEZO KUHUSU PROGRAMU YA AFDP
NA, MWANDISHI WETU - DODOMA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, chini ya Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Edwin Swalle, imejengewa uelewa kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na kusimamiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu na kuipongeza Ofisi hiyo kwa namna inavyoratibu na kuhakikisha Programu inayafikia malengo kwa tija ya Taifa kwa ujumla.
Akizungumza baada ya semina fupi iliyoandaliwa na Ofisi hiyo, Mheshimiwa Swalle amesema mradi wa AFDP umefanikiwa kuwafikia wananchi wengi kupitia ukuzalishaji wa mbegu bora za Kilimo, kilimo cha zao la mwani na uzalishaji wa vifaranga vya samaki, hatua inayochochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha Wakurugenzi wa Halmashauri ili kubaini mahitaji halisi ya wananchi na kuhakikisha mradi huo unawanufaisha watu wengi zaidi na kuendelea kuwa na tija kwa jamii.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mheshimiwa Ummy Nderiananga amesema utekelezaji wa Mradi wa AFDP umeshirikisha wadau mbalimbali wa wizara za kisekta kuanzia Makatibu Wakuu ili kuleta maendeleo endelevu ya utekelezaji wa Mradi wa AFDP
Semina hiyo imelenga kuwajengea uelewa Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi wa AFDP.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Post a Comment