TANFORD kuwa kutanisha wadau sekta ya biashara
Vijana wa Tanzania kuchangamkia fursa. baada ya Kampuni ya TANFORD Business Administrative Services L.L.C iliyopo Dubai kuwa imeandaa Kongamano la Kimataifa (Tanzania Trade and Logistics Forum 2026) litakalowakutanisha wadau muhimu wa biashara.
Ambapo kufanyika , kutawezesha uwekezaji, usafirishaji na uchumi kutoka Tanzania, United Arab Emirates (UAE), Afrika Mashariki, GCC na nchi zisizo na Bandari( Land Locked Countries).
Akizungumzia na Waandishi wa habari leo Desemba 16,Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw.Hussein Jamali amesema Tanzania nikitovu cha Biashara cha ukanda wa Afrika Mashariki.
Lengo la Kongamano limetajwa kuwa litachagiza kutangaza fursa zilizopo Tanzania,ikiwa ni pamoja na Mamkala ya Bandari Nchini (TPA), Shirika la Reli Nchini( TRC), Mamlaka ya Anga (TAA), Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Nchini (TANTRADE), Mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalumu ya kiuchumi(TISEZA), Mamlaka ya kukuza uwekezaji Zanzibar(ZIPA), amesema Jamali.
Amesema Kongamano hilo la kibiashara Tanzania linatarajiwa kufanyika January 13 hadi 14 mwakani 2026 Dubai ambapo vijana wa Tanzania watatakiw kuchangamkia fursa.
Jamal amesema malengo mengine ya Kongamano hilo ni pamoja na kujenga majukwaa ya ushirikiano kati ya Sekta binafsi na Serikali kwa ajili ya mikataba,ubia na ujenzi wa miradi ya kimkakati,kuunga mkono makampuni ya Cargo,Clearing & Forwarding na Logistics kwa kuyakutanisha na masoko mapya ya UAE,GCC na Asia.
Vile vile amesema kuwa washiriki wa Kongamano hilo ni pamoja na Taasisi za Serikali na Makampuni ya Sekta binafsi kutoka Tanzania na UAE ,GCC,Asia na Afrika,Taasisi za kifedha,wawekezaji wakubwa na wawekezaji binafsi(Angel Investors & Venture Capital),Nchi zisizo na Bandari,wadau wa Cargo,Logistics, Shipping and Supply chain,pamoja na Vijana wa Tanzania kupitia Youth Innovation & Business Stage.
Aidha, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Maroli ya Mizigo Nchini (TATOA) Elias Lukumay amesema kuwa kumekuwa na Changamoto kwa Vijana katika kuzibaini fursa na kuzichangamkia fursa za kibiashara.
Amesema kupitia Kongamano hilo , nifursa nzuri kwa vijana kukuza Bishara ili kukuza Umahiri na Ufanisi katika sekta hiyo.
"Kongamano hili litawezesha ukuaji wa Biashara na ufanisi wa Bandari Congo,Zambia, Burundi "Amesema Mwenyekiti wa TATOA Elis Lukumay.
Naye ,Rais Tanzania Fraught Foward Association (TAFA)Edward Urio amesema shirikisho hilo lina jumla ya makampuni Takribani 1400 Ambapo amesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika Dubai unaumuhimu wakipekee.
Hivyo amebainisha sekta ya Usafirishaji wa mizigo ndio chanzo kikuu cha Fedha za kigeni.

Post a Comment