Ads

Wadau mbalimbali wamekutana katika mkutano wa kujadili mustakabari wa uhifadhi wa Matumbawe


Meneja hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu ,Davis Mpotwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uhifadhi wa Matumbawe pembezoni mwa mkutano wa waduu wa uhifadhi mazingira na Matumbawe.

Na. Mwandishi wetu

No mustakabari wa uhifadhi wa Matumbawe na utekelezaji wa  wa mradi wa okoa Matumbawe

Akizungumza na waadishi wa habari Leo Oktoba 7,2025 Jijini Dar es Salaam Meneja hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu ,Davis Mpotwa , amesema kwamba Tanzania ni Moja ya nchi ambayo ina aina ya  matumbawe  yanatopatikana katika Ukanda wa magharaibi mwa bahari lakini kwa ujumla katika nchi saba zinazitekeleza mradi huu wa okoa matumbawe.


""Kikao Cha Leo kinalenga kutoa fursa kwa watanzania kujifinza juu ya uhifadhi wa matumbawe kupitia usomaji wa kimtandao unaweza kujisajili kupitia mtandao kwa kushare link kutoka taasisi mbalimbali za serikali wa wataendae katika vyuo vyao na mashirika  yao kuhakikisha  kwamba  kijana wakitanzania  wanapata fursa ya kusoma kozi za online zinazohusu matumbawe jinsi gani yakuhifadhi matumbawe na kutumia taaluma za kisayamsi kuhakikisha matumbawe yanaendwa  na kuhifadhiwa" Amesema 


Pia amesema kuhakikisha mazalia ya samaki yanaendelea kuwepo kwa kizazi Cha Sasa  na  kijacho na kuthamini kile ambacho  wamefanya katika miaka hii mitatu iliyopita katika utekelezaji wa mradi kwa pamoja  wanaenda kutekeleza mwaka wa nne katika kipindi hiki.


Hata hivyo amesema yapo mambo ambayo  wamekunalina kuyafanya ikiwa ni pamoja na kutengeneza mfumo portal,  ambao utasaidia wanasayansi wote  wanahusika na masuala ya baharini hususani katika masuala ya matumbawe kuwa sehemu ambayo wanahifadhi taarifa zao  pamoja na kupakua taarifa  kutoka  sehemu mbalimbali duniani na kuzitumia kwa ajili yakuhakikisha kwamba jamii inazipata.


Sanjari na hayo pia amewaasa waandishi wa habari pamoja na jamii nyingine wanakua nafursa ya kuingia  katika mfumo portal kupata taarifa mbalimbali hususan zinazohusu bahari,uchafuzi wa mazingira ili kuwa natakwimu halisi unapotoa kwenye vyombo mbalimbali kama magazeti,tovuti au sehemu mbalimbali kama  majukwaa  kwa ajili ya jamii.


Ametoa wito kwa jamii kutembelea katika maeneo yanayohifadhi matumbawe. Tanzania ni nchi mojawapo ambayo imehifashi vizuri sana matumbawe yake na kwa kiwango kikubwa hivyo Gf7 wameona ni maeneo ambayo yanafaa kufadhiliwa kuendelea kuhifadhi maeneo haya ambayo kwa muda mrefu yamekua katika hali yake nzuri kama Tanga,Pemba,Unguja,Kilwa,Mtwara na Dar es Salaam.

Mradi huu Tanzania inaongoza katika utekelezaji wake katika nchi Saba .


Naye Mtafiti na mwalimu kutoka Chuo Kikuu Cha kilomo Cha sokoine Rose Kicheleri  amesema mradi umewasidia  kupata taarifa muhimu ambazo zitasidia  sana kufanya maamuzi ya uhifadhi wa matumbawe pamoja na kuendeleza matumbawe katika nchini .

Amesema  wamehusika katika  tafiti mbalimbali na kupata taarifa ambazo ni nzuri na zote zinasaidia  hasa tafiti za matishio na fursa  ambazo zinatokana na Matumbawe hasa uelewa wa wadau kutoka ngazi tofauti kuhusu matumbawe,  mfano matishio na fursa nyingi sana hizi zinaendana na uchimi wa Buluu  kwa Tanzania bara  bado hazijaweza kuchukuliwa  na wadau mablimbali lakini kwa Zanzibar fursa hizi zinachukuliwa kwa nguvu.

 Hivyo  amesema  ufanyaji wa maamuzi taarifa hizi zinasaidia katika  kutekeleza sera za nchi ili kuweza kuweka nguvu zaidi na nikwa jinsi Gani nchi inaweza kufaidika na haya matumbawe.

"Matishio ni kazi za kibinadamu pamoja na mabadiliko ya tabianchi hizi zinakua katika kazi tofauti kutika ngazi ya chini kabisa kwa wananchi wanatumia matumbawe kupata samaki.


Ameongeza kwa  kusema kwamba uelewa wa wadau hasa wananchi unahusiana Moja kwa Moja na matumbawe Wana uelewa mkubwa wavuvi na wale wanaohusiana kama wizara ya uvuvi na mifugo,taasisi zisizo za kiserikali na wadau wengi sana hawana uelewa tunatumia samaki hovyo kunahitajika kuonyesha umuhimu wa kuongeza uelewa wa wadau katika ngazi tofauti kuhusi matumbawe


Kwa upande wake Afisa uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi, Upendo Hamidu amesema kwamba  wanaangalia ushiriki wa makundi maalumu  hasa wanawake na vijana kwenye kusimamia Matumbawe hasa athari  zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia shughuli za tabia nchi zinayaharibu .

Amesema mazalia ya samaki yanasababisha kutupatia kiapato pamoja na ulonzi wabahari lakini chamgamoto zinaathiri wadau mbalimbali waliopo kwenye jamii.


Pamoja na hayo amesema kuwa  utafiti tuliofanya kuhusu uelewa wa Matumbawe kwa upande wa wanawake wengi sio waelewa kwasababu wao mara nyinginwanabaki pwani hawaendi kuvua samaki,wakati jaamii wanapokea samaki lakini wao katika Jambo la uharibifu kwa Matimbawe hivyo wanaanda program maalumu  zitakazosaidia uelewa  wanawake na program ambazo zitakuwa endelevu na yanaendelea kutoa faida zinazotokana na  Matumbawe kwa taifa Zima lakini  wao wenyewe na jamio kwa ujumla.









No comments