RC CHALAMILA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA
Na mwandishi wetu
Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Albert Chalamila amewata wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29,2025 ili kutumia haki Yao ya msingi ya kikatiba kwa kushiriki kikamilifu kuchagua viongozi wanaowataka
Hayo ameyabainisha Leo Oktoba 27,2025 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa Moja asubuhi na kufungwa saa 10:00 kamili jioni.
Aidha ,RC Chalamila amewatoa hofu wananchi na kusema kwamba Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mwananchi anapata nafasi ya kutumia haki yake ya kikatiba ya kupiga kura bila hofu wala vurugu kwakua Serikali inatambua kuwa suala hilo ni haki ya kikatiba
Sanjari na hayo, amevitaka vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi bila kufanya upotoshaji kwani vyombo vya habari ni muhimuli muhimu ambao ni kiunganishi kati ya wananchi na Serikali yao ambapo ametumia pia nafasi hiyo kuwataka viongozi kuanzia ngazi ya mitaa kulinda miundombinu ya Serikali ikiwemo ya umeme na barabara za mwendokasi ambapo amisisitiza barabara hizo kutotumiwa na vyombo vingine vya usafiri
Sambamba na hayo amewataka wakazi wa mkoa huo kupuuza taarifa za uzushi zinazotolewa na baadhu ya watu kupitia mitandao ya kijamii kuwa uchaguzi utakua na vurugu amewahakikishia kuwa mkoa uko salama sana wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Post a Comment