Ads

WAGOMBEA CCM WOTE WALIOKATWA WAREJESHWA KUPIGIWA KURA NA WAJUMBE.

 

Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imewaelekeza Makatibu wa Mikoa wa CCM wote nchini kuhakikisha wagombea wote wa udiwani wa kata, waliopitishwa na Kamati za Siasa za mikoa wanarejeshwa ili wakapigiwe kura za maoni.

Pia imeelekeza wagombea wote waliopo kwenye orodha ya awali waliyotumiwa Makatibu wa Mikoa wa CCM, warejeshwe ili wakapigiwe kura za maoni.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo AgostI 1, 2025 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla imesema
hatua hiyo imetokana na uamuzi wa kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika Alhamisi Julai 31, 2025, kujadili kwa kina malalamiko yaliyojitokeza katika mikoa mbalimbali nchini.

Aidha, kikao hicho kimefuta maelekezo yote yaliyotolewa awali hivyo kuwaelekeza Makatibu wa Mikoa wa CCM wote nchi nzima, kuzingatia na kutekeleza maelekezo ya sasa.

No comments