CCM MKOA WA DAR ES SALAAM WATANGAZA MAJIN YA MADIWANI WATEULE KATA NA VITI MAALUMU
DAR ES SALAAM
KATIBU wa Siasa,Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Dar es Salaam,Ally Bananga,ametangaza majina ya uteuzi wa wagombea nafasi ya udiwani na viti maalum Mkoa Dar es Salaam.
Majina hayo yametangazwa leo Agosti 14,2025 mara baada ya zoezi hilo kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kujadili na kufanya uteuzi wa mwisho ya wagombea watakaokwenda kukiwakilisha Chama cha Mapinduzi kwenye Uchaguzi Mkuu.
Aidha ,amesema kwamba kwa ujumla kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam kiliazimia na kuteua kwa asilimia 99.2 wagombea waliongoza kwenye kura za maoni katika kata zote 102.Hata hivyo,katika kata ya Vijibweni kutokana na changamoto mgombea aliyeongoza kura za maoni hakuteuliwa hivyo kufanya asilimia 0.98 ya waliongoza kura za maoni kutoteuliwa.
"Uteuzi huu umezingatia Kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya Dola,Kanuni ya 9(1) inayosema"Mgombea yoyote wa CCM anayetaka kuingia katika chombo Cha Dola,atateuliwa kwa kuzingatia kura za maoni zilizopigwa.Mgombea atakayeteuliwa ni yule anayeongoza kwa wingi wa kura za maoni alizopata.Isipokuwa kwamba endapo itathibitika kuwa kura hizo za ushindi amezipata kwa njia ya rushwa,kikao Cha uteuzi wa mwisho hakitamteua mgombea nafasi aliyoomba",amesema Bananga.
Hata hivyo,ametaja mchanganuo wa uteuzi wa wagombea katika Wilaya 5 na kata 102 za Mkoa wa Dar es Salaam
Pia amesema kwamba uteuzi wa wagombea walioteuliwa ni asilimia 50.98 ni ya wagombea wapya na asilimia 49.02 ni ya wagombea wa zamani kwa hiyo mchakato huu umezingatia demokrasia ndani ya Chama Cha Mapinduzi
Sambamba na hayo katika uteuzi wa wagombea Wilaya ya Ilala ina majimbo 4,Kata 36 katika Jimbo la Ilala Lina Kata 10 wameteuliwa wagombea wa zamani ni 7 na wapya wagombea 3.
Pia ametaja Jimbo la Kivule Kata ziko 6 wagombea wa zamani 3 na wagombea wapya 3.
Katika Jimbo la Ukonga lina kata 7 wagombea wa zamani ni 1 na wagombea wapya 6.
Aliongeza kwamba Jimbo la Segerea ziko kata 13 wagombea walioteuliwa wa zamani ni 7 na wagombea wapya 6 pamoja na kusema kuwa Wagombea wa Udiwani Viti Maalum wako 14 .
Aliendelea kwa kutaja majina Wilaya ya Temeke Kata 23 kwa kusema kuwa Jimbo la Temeke Kata 13 wagombea wa zamani ni 11 na wagombea wapya 2 na kwa upande wa Jimbo la Mbagala Lina kata 6 wagombea wote ni wapya.
Jimbo la Chamazi Lina kata 4 wagombea wapya 3 na 1 wa zamani ambapo Jimbo la Kigamboni lenye kata 9 wagombea wapya 3 na wazamani 6.
Alithibitisha katika Wilaya ya Ubungo Lina Kata 14 ambapo Jimbo la Ubungo Kata 8 wagombea wa zamani 4 na wapya 4 ,aidha Jimbo la Kibamba Kata 6 na wagombea 6 wote wapya.
Alimalizia kwa kutaja wagombea walioteuliwa kataka Wilaya ya Kinondoni yenye Kata 20 ambapo katika Jimbo la Kinondoni lina kata 10 wagombea wa zamani 5 na wapya 5 na Jimbo la Kawe lina Kata 10 wagombea wa zamani 2 na wagombea wapya ni 8
Post a Comment