TIRDO YAJA NA MBINU YAKUTENGEZA MKAA MBADALA
Na Angelina Mganga
DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO) liko chini ya wizara ya viwanda na biashara ambalo linajihusisha na tafiti za kusaidia viwanda na lilianzishwa mwaka 1979 na Makao Makuu yapo Msasani Jijini Dar es Salaam.

Tembelea Banda la TIRDO katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara(SABASABA) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtafiti na Mtaalam wa Mazingira TIRDO,Kunda Sikwaze akielezea jinsi gani wanavyofanya tafiti mbalimbali kuhakikisha wanatengeneza nishati safi ,katika kipindi msimu huu wa maonesho mwaka huu wamewaletea jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala.
Akifafanua kwa undani kuhusu mkaa mbadala leo Juni 5,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa habari Mtaalamu Kunda amesema kwamba mkaa mbada unatengenezwa kwa kutumia mabaki ya mazao mbalimbali na mabaki ya misitu ikiwemo mabaki ya vifuu vya Nazi,pumba za mpunga pamoja na chikichi za mawese.
"Pumba za mpunga kiwango chake sio kizuri sana kwa sababu ya jivu jingi na kiwango cha joto ni kidogo ili kupata mkaa wenye ubora lazima kuchanganya pumba za mpunga na vifuu vya nazi ili kupata viwango vinavyokubalika ",amesema Mtafiti Sikwaze
Aidha ,amesema kwamba pumba za mpunga na vifuu vya nazi vinawekwa kwenye tanuu la kuchomea mkaa lililotengenezwa ili kuzuia uchafuzi wa mazingira,moshi unaotoka unapitishwa kwenye kifaa maalum na joto linalorudishwa linatumika kama mkaa mbadala.
Pia amesema kifuu kinapochomwa yaani malighafi hiyo ina chomwa kwa kiwango kidogo ambapo kinapatika kiwango kidogo Chakupata hewa ya oksijeni ambapo haki unguu ndipo mpaka kutokea majivu bali kinaungua kiasi .
Hata hivyo,amesema kwamba baada ya kusaga unapatikana unga ambao unachanganywa na kiunganishi kwa utafiti uliofanyika ,ambacho ni uji wa unga wa muhogo na kinatoa marighafi nzuri zaidi na inapitishwa kwenye mashine kwa ajili yakupata maumbo mbalimbali kama umbo la duara mfano wa kitumbua na tunaweza kutumia kwenye majiko ya kawaida na maumbo makubwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
Post a Comment