Mkinga Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam ; miundombinu ya barabara nimuhimu kutunzwa vizuri
Na Francisco Peter, Dar es Salaam
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imesema miundombinu ya barabara nimuhimu kutunzwa vizuri hivyo imekuwa ikishirikiana na jamii katika maeneo yenye miradi.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Geofrey Mkinga
amesema Wakala umeimarisha upitikaji wa miundombinu ya barabara za wilaya zenye urefu wa kilometa 5,057.765 .
"Tumewai kufanya kampeni ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza miundombinu ya barabara kwa kuepuka kutupa taka ngumu kwenye mitaro kupitia kaulimbiu yake ya "Mitaro Sio Jalala".
Amesema mafanikio hayo yametokana na ongezeko kubwa la bajeti ya TARURA kutoka shilingi bilioni 25.431 hadi shilingi bilioni 52.334 sawa na ongezeko la asilimia 205.79 kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2024/25.
“Mtandao wa barabara za lami katika kipindi hichi umeongezeka kutoka Kilometa 450.29 hadi Kilometa 677.04, na changarawe kutoka Kilometa 1616.22 hadi Kilometa 1898.82 huku
barabara za udongo zimepungua kutoka Kilometa 2990.49 hadi Kilometa 2481.14 kwa mapato ya ndani,” amesema Mhandisi Mkinga.
Aidha Mkinga amesema TARURA imewahi kufanya kampeni hiyo katika Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam na kutolea mfano wameisha wahi kushirikiana na Wilaya ya Kinondoni ambapo walikutana na kupanga mkakati wa kutunza mitaro inayojengwa katika barabara Wilayani humo.
"Tulikutana na kufanya kikao cha pamoja kati ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Meneja wa TARURA Mkoa wa wa Dar es Salaam pamoja na Timu ya Kitengo cha Mazingira kutoka TARURA Makao Makuu.
Mkinga ameeleza umuhimu wa utunzaji wa mitaro na barabara kwa ujumla na kusisitiza kuwa jambo hili si la TARURA pekee bali linahusisha uongozi kuanzia ngazi ya wilaya, mitaa na wananchi ambao ndio wanaoshiriki kutupa taka katika mitaro na kusababisha mafuriko na magonjwa ya mlipuko.
"Zipo sheria zinazohusu utanzaji wa barabara, mazingira na afya na sheria hizi zipo chini ya usimamizi wa Halmashauri ambapo Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya ndio wenye jukumu hilo, hivyo kwa kushirikiana tunaweza kufanikisha vizuri zoezi hili", alisemaMkinga.
Aidha, wataalamu wa mazingira wamewasilisha sheria mbalimbali zinazo bainisha sera, sheria na vifungu vinavyoelezea namna ya kutunza mazingira pamoja na adhabu za ukiukwaji wa sheria hizo.
Ata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saadi Mtambule alishaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha akishirikiana na wasaidizi wake katika kufanikisha zoezi hilo.
"Tunashukuru kwa jitahada na ushirikiano mnaoendelea kutupa mara kwa mara, sisi ni serikali na ni wajibu wetu kutunza na kusimamia rasilimali zote za serikali tukishirikiana wadau na wananchi kwa ujumla.
Vilevile ameeleza kuwa wao kama wilaya wamekua na kampeni ya kufanya usafi kwa muda Sasa.
"Baadhi ya wananchi wamekua wakijitokeza kwa ajili ya usafi na utunzaji wa barabara na katika maeneo mengi wananchi wameendelea kutoa ushirikiano katika kufanya usafi". Alifafanua Mhe. Mtambule
Mhe. Mtambule aliendelea kusema kuwa Kinondoni imekuwa na mikakati ya kushirikiana na wadau kutoka ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha swala la usafi katika wilaya ya Kinondoni inazidi kuwa safi hasa katika maeneo ya mama lishe.
Post a Comment