Ads

MHE.KIGAHE AWATAKA TIRDO KUENDELEA KUTOA ELIMU JUU YA MATUMIZI YA MKAA MBADALA.

 

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe amewataka wataalam wa TIRDO kusambaza teknolojia na elimu juu ya uzalishaji wa Mkaa mbadala kote nchini.

Mhe.Kigahe ameyasema hayo alipotembelea banda la TIRDO katika Maonesho ya Biashara za Kitamaifa Dar es salaam maarufu kama sabasaba. Naibu waziri huyo aklifurahishwa na teknolojia hiyo ambayo kwa kiwango kikubwa inasaidia katika kupunguza ukataji miti pamoja na kuhakikisha 

wananchi wanapata nishati salama na isiyoharibu mazingira.

Niwapongeze sana kwa hatua hii lakini hakikisheni hii teknolojia inawafikia watu wengi ili sisi kama wizara ya Viwanda na Biashara tuwe sehemu ya watunza mazingira lakini pia kuunga mkono juhudu za Mhe.Rais wa  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara katika mapambano ya utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati mbadala ya kupikia’’ aliongeza Mhe.Kigahe

Mtaalam wa Mazingira kutoka TIRDO Bi.Kunda Sikazwe amemuelezea Naibu waziri kuwa mpaka sasa TIRDO imetoa mafunzo kwa wazalishaji kutoka

mikoa 12 kwa Tanzania bara ambapo wazalishaji hao walipatiwa elimu juu ya namna ya kuzalisha mkaa , uchanganyaji, pamoja na mali ghafi inayotumika katika uzalishaji.

Katika Maonesho ya 49 ya Sabasaba TIRDO wanashiriki kwa kutoa elimu juu ya matumizi ya mkaa mbadala unaotokana na vifuu vya nazi, maganda ya michikichi, pumba za mpunga pamoja na kutoa elimu juu mnyororo mzima wa matumizi ya nishati unaoanzia aina ya nishati , aina ya jiko pamoja tabia ya mtumiaji.

Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanaendelea katika 

viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tangu tarehe 28 Juni hadi Juali 13, 2025.










No comments