Ads

Mama Janeth Magufuli Atembelea Banda la TCCIA Sabasaba

Mke wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,awamu ya(5) John Magufuli, Mama Janeth Magufuli (kushoto) akisikiliza maelezo ya  Afisa biashara wa Chemba ya biashara,Viwanda na kilimo Tanzania(TCCIA), Fatma Khamis alipotembelea banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba jijini Dares Salaam leo. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa TCCIA.


Bandani hapo, Mama Janeth alisaini kitabu cha wageni na kupokea maelezo kuhusu huduma na jitihada mbalimbali za TCCIA katika kuendeleza biashara, viwanda, na kilimo nchini. Amepongeza mchango wa TCCIA katika kuhamasisha maendeleo ya sekta binafsi na kuinua uchumi wa taifa pia aliwataka wananchi kutembelea banda hilo ili kujifunza namna mbalimbali za kufanya Kilimo biashara kutika kwa Washauri  waliopo katika taasisi hiyo.

Mjane wa Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli, ametembelea Banda la Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yanayoendelea jijini Dar es Salaam.



No comments