Ads

WANANCHI WAOMBA HUDUMA ZA KISHERIA ZA MAMA SAMIA ZIWE ENDELEVU.




Kampeni ya msada wa kisheria wa Mama Samia (Mama Samia legal Aid campaign) inayoendelea katika viwanja vya Maturubai Mbagala Kizuiani Wilayani Temeke hapa Jijini Dar es salaam imeshika kasi ambapo wananchi wengi wameendelea kujitokeza kupata huduma za kisheria.


Baadhi ya wananchi waliofika leo June 19 kupata huduma za kisheria  katika banda la ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali wameielezea kampeni hiyo kuwa ni Mkombozi kwani wamepata msaada wa kutatua matatizo yao ya kisheria ambayo yalishindikana kutokana na kukosa gharama za kumlipa Wakili atakaye watetea ili wapate hakizao kisheria.



Akizungumza aliofika kuapata huduma  katika Banda la huduma la Mwanasheria mkuu wa Serikali,  Mercy Mahenge, ambaye ni mwananchi wa kawaida ameishukuru Serikali  na kusema kuwa shukrani zake zifike mojakwa moja kwa  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye aliona kunahaja ya kusogeza uduma hizi za kisheria katika ngazi ya chini kwa  wananchi wa kawaida.


Amesema  kwa hali yakawaida nivigumu kumpata Mwanansheria lakini kwa sasa imekuwa rahisi kutembea tu mpaka hapa uwanja unakutana na Mwanansheria na kueleza shida yako.


''Kwahii Sehemu ambayo naweza nikatembea nikafika kirahisi na nikakutana na wataalamu wa sheria, kwangu mimi nimeona nikitu kizuri kinatakiwa kiwe endelevu kwaajili yetu sisi wananchi kimetusaidia Zaidi"Amesema Mercy.


''Mimi naitwa naitwa Dorcas Cyprian, naishukuru Serikali kwa hii kampeni sababu tumehudumiwa kisheria na imekuwa rahisi kwetu  sisi wananchi wa hali yachini hatupati gharama ya kumuona Wakili wa Serikli tunamshukuru sana Mama Samia huduma hii iendelee.Amesema Dorcas


Aidha baadhi ya Wananchi waliofika katika banda la Mwanasheria mkuu wa Serikali ambao hawakutaka majina yao kutajwa wameshauri vyombo vya Habari kutangaza mambo mazuri kama haya ambayo Serikali inayatoa kwa raia wake  ili kuwatia moyo watu wote ambao wamejitoa kwa moyo kuhudumia na kusaidia juhudi hizi za Rais Samia kuigusa jamii moja kwa moja katika matatizo na changamoto zao kisheria.

 











No comments