Ads

EWURA yasifiwa Kufanya kazi Kubwa Miradi ya Kimkakati

Na Francisco Peter 

Serikali imesifia EWURA kuwa imefanya kazi kubwa kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa zilizopo katika miradi ya kimkakati kama EACOP. 

Zaidi ya hapo , mfumo thabiti unatajwa kuwa umechangia utulivu wa bei katika sekta zote za nishati na maji na pia mbinu za ufuatiliaji za kuhakikisha marekebisho yoyote ya bei zinazopendekezwa zinapitia mchakato wa uhakika wa kina unaohusisha mashauriano ya umma.

Mbinu hiyo ya mashauriano inaruhusu watumiaji kutoa maoni yao na hivyo kuimarisha uwajibikaji.

Katika utekelezaji mwema tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni usimamizi wa mamlaka katika sekta ya umeme ikiwemo nishati jadidifu, kuunga mkono miundombinu mipya, na kuhamasisha upanuzi wa upatikanaji wa umeme na kuboresha huduma za maji kitaifa.

Kwa sasa, EWURA inaeendelea kuwa taasi muhimu katika sekta za huduma za nishati na maji kwa umma nchi Tanzania huku ikitumia changamoto kama fursa mpya na kuhakikisha kuwa huduma za nishati na maji zinatolewa kwa ufanisi.

Mara kwa mara EWURA inatathimini watoa huduma kulingana na viwango vilivyowekwa ambapo ungalizi huo wa mapema EWURA inapambanua husaidia kubaini na kushughulikia masuala mbali mbalimbali, na imetoa njia ya wazi inayopatikana kwa kila anayehitaji utatuzi wa malalamiko yake.

Hali hiyo imeifanya serikali Kuendelea kusimamia sera za ushiriki wa wazawa ili kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa kwa kuwa zinawanufaisha wananchi wake.

"Naipongeza sana kwa kazi hii kubwa inayoendelea . Niwahakikishie kuwa Serikali itaendelea kusimamia sera," hayo yalisemwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko 

Biteko alitoa pongezi hizo , Machi 24, 2025, wakati akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ambao walisisitiza umuhimu wa kuhakikisha Watanzania wanapewa kipaumbele cha ajira katika miradi mikubwa ya kimkakati.

Akizungumzia mchango wa EWURA, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa kuhakikisha sera na miongozo ya ushiriki wa wazawa inatekelezwa kwa ufanisi, hali iliyowezesha Watanzania kunufaika na fursa za ajira na zabuni katika miradi hiyo.

"EWURA imefanya kazi kubwa kuhakikisha Watanzania wananufaika na fursa zilizopo katika miradi ya kimkakati kama EACOP.

Naipongeza sana kwa kazi hii kubwa inayoendelea kufanya. Niwahakikishie kuwa Serikali itaendelea kusimamia sera za ushiriki wa wazawa ili kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha wananchi wake," amesema Dkt. Dk. Biteko.

Aidha, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya nishati ili kuimarisha ushiriki wa wazawa katika miradi yote inayoendelea na inayotarajiwa kuanza kutekelezwa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile, awali Alisha sema uamuzi wa serikali kuachana na ukodishaji wa mitambo ya kuzalisha umeme katika miaka ya nyuma umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa hali ya kifedha ya TANESCO.

Ambapo taarifa za maendeleo ya sekta ya nishati kwa mwaka 2023/24, Dkt. Andilile alisema hapo awali, mitambo ya kukodi ilisababisha ongezeko kubwa la bei ya umeme, ikiwemo asilimia 40 mwaka 2011 na asilimia 39 mwaka 2013, kutokana na migogoro ya mkataba na kutopunguzwa kwa bei ya huduma.

Aidha, alibainisha kuwa baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya serikali, ikiwemo ya Kinyerezi na Bwawa la Julius Nyerere, EWURA imepanga kufanya utafiti wa kina kuhusu gharama halisi za utoaji wa huduma kwa mwaka wa fedha ujao.

Kwa upande wa sekta ya mafuta, Dkt. Andilile amesema hadi kufikia Juni 2023/24, jumla ya vituo vya mafuta vilivyokuwepo vilikuwa 2,361 sawa na ongezeko la asilimia 10, huku vituo vilivyoko vijijini vikiwa 480, ongezeko la asilimia 12.


Hata hivyo, ameeleza kuwa licha ya changamoto zilizotokana na siasa za kidunia na mabadiliko ya sera za kiuchumi za Marekani mwaka 2022/23, upatikanaji wa mafuta nchini umeendelea kuwa wa uhakika.

No comments