BENKI YA AKIBA YAZINDUA KAMPENI YA 'TUPO MTAANI KWAKO'
Wito huo ameutoa Septemba 21, 2024 Dar es Salaam Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango wakati akizindua rasmi kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo , Letsya Tower ambapo amesema wapo mtaani kila mahali wakitoa huduma ikiwemo elimu ya mikopo, jinsi ya kutumia huduma za kidigital VISA card,ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking.
”Tumezindua rasmi program yetu ya Tupo Mtaani Kwako kupitia timu yetu bobezi ya mauzo sasa tunakufika popote ulipo nchi nzima kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti , elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking” amesema Afisa biashara
Muyango amesema Program hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya “Tupo Mtaani kwako” katika vitongoji na mitaa mbali mbali ya jiji la DSM
.
Post a Comment