MAENDELEO BENKI SAINI MKATABA KUWASAIDIA WAMACHINGA DSM
Na Fransisco Peter, Dar es Salaam
Mandeleo Benki Leo imesaini mkataba wa makubaliano ya pamoja Kati yake na shirikisho la umoja wa wamachinga wa Kariakoo (KAWASSO) utakaowawezesha wafanyabiashara hao kupata viwanja vya makazi sambamba na kupata mikopo kwa ajili ya Kujengea nyumba unaojulikana kama 'Machinga Plot Finance'
Akizungumza na waandishi wa habari Leo May 7,2024 Mkurugenzi wa benki hiyo amesema kuwa kupitia Mkataba huo,Benki hiyo itatoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya milioni 500 kwa wamachinga karibu 500 kwa awamu ya kwanza ili kuwawezesha kumiliki viwanja hivyo.
Amesema kuwa pesa hizo zitakuwa kwa ajili ya ununuzi wa ardhi,usafishaji wa eneo husika,upimaji wa viwanja na urasimishaji ili kuwezesha mgawanyo wa viwanja kwa wanachama binafsi ili kila mnufaika aweze kuwa na hati yake.
"Mandeleo Bank PLC,tulipokea maombi kutoka Kawasso ya ujenzi wa nyumba za makazi kwa wamachinga ambapo tulikubaliana kuanza na ununuzi wa viwanja na hivyo kuwawezesha machinga wa Mkoa wa Dar Es Salaam kumiliki viwanja na hatimaye kupata makazi ya kuishi,na umoja huo tayari umeshapata hekari 89 katika Kijiji cha Magoza kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani" amesema na kuongeza kuwa,
Benki hiyo imeamua kuja na Mpango huo kwa kutambua changamoto zinazowakabili wajasiriamali wadogo na watu wenye makundi maalum kama la wamachinga kuwa ni ukosefu wa dhamana zinazowawezesha kupata mikopo kwa ajili ya mitaji kupitia taasisi za fedha ambapo Benki iliamua kuridhia ombi la Machinga la utoaji wa mikopo ya Nyumba kwa kuanza na viwanja.
Hata hivyo katika hatua nyingine Benki hiyo kwa kushirikiana na Kariakoo Wamachinga Association (KAWASSO) ili kufanikisha lengo Hilo la mikopo,imeingia makubaliano ya pamoja na mmiliki wa eneo husika watakapojenga wafanyabiashara hao pamoja na makubaliano mengine na kampuni ya urasimishaji ardhi ya Semsic Land Consultant Limited itakayowawezesha wamachinga Mkoa wa Dar Es Salaam kupata viwanja vya bei nafuu isiyozidi milioni 1 kwa kiwanja kimoja huku wakirejesha kidogokidogo kwa muda wa miezi 12.
"kukamilika kwa Mpango huu,kutawawezesha wamachinga kumiliki ardhi na makazi bora,na pia kutawaongezea sifa ya kukopesheka zaidi ili kukuza mitaji na hii yote tunafanya kwa kuitikia kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa kupambania makundi maalum ikiwemo Wamachinga,vijana na wanawake kwani pia tunatoa mikopo ya Bajaj kwa vikundi ambavyo haihitaji dhamana zaidi ya Chombo chenyewe"alisema
Post a Comment