Ads

VUNA DEILE YATOA FURSA KWA VIJANA KIJIKWAMUA KIUCHUMI

Na Francis Peter, Dar es Salaam

Kampuni ya Three Oceans Ltd. Inayojishughulisha na uendeshaji wa mchezo wa kubashiri wa VUNADEILE  imewataka vijana kuchangamkia fursa kwa kushiriki mara kwa mara michezo kubashiri kwa ajili ya kujipatia vitu mbalimbali ikiwemo usafiri wa gari au pikipiki, fedha ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumia pamoja na  kujikita katika shughuli za kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow - BBT) ambao wameonesha nia ya kuwasaidia.

Akizungumza leo Aprili 22, 2024 jijini Dar es Salaam Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Mawasiliano kutoka kwenye kampuni hiyo Naseem Alla wakati akiwatangaza washindi wa Vuna Deile baada ya kuchezeshwa droo ya kwanza, Naseem Allan, amesema kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa kwa shiriki michezo ya  kubashiri kama fursa ambayo itawasaidia kufikia malengo.

Allan amesema kuwa mchezo wa Vuna Deili inatoa fursa kwa mtu yoyote mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na kucheza na kushinda vitu mbalimbali gari mpya kabisa aina ya Toyota Ist, pikipiki, tv na simu janja aina ya Samsung na iphone 15.

Amesema kuwa katika kuendesha bahati nasibu hiyo kampuni inashirikiana na Mradi wa kilimo ili kuhakikisha tunawawezusha vijana-BBT ni Taasisi iliyopo chini ya wizara ya kilimo yenye lengo kuu la kutoa hamasa kwa Vijana kujikita kwenye shughuli za kilimo biashara Ili waweze kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.

"Cheza mara nyingi zaidi kila siku ili uweze kujihakikishia nafasi ya kushinda ni mwendo wa kumiliki ndinga na kupiga pesa kila siku, Panda buku vuna GARI Ndio maana tunasema VUNA DEILE“ amesema Allan.

Amesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali katika kuwawezesha Vijana kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri.




Mratibu wa Maradi programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow – BBT)  ambayo imejikita kuwasaidia vijana katika sekta ya kilimo, Vumilia Zikankuba, amesisitza umuhimu wa vijana kujiunga katika programu hiyo ili waweze kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.


No comments