Ads

Zali atua nchini Kuongeza Mkataba wa bidhaa za softcar

Na Francisco Peter

Aliye wai  kuwa mpenzi wa mwanamziki Nasbu Abdul(  Doamond)   Zari Hassan kwa jina maarufu (Boss lady ) ameongezewa tena mkataba wake wa kutangaza bidhaa zinazozalishwa na Kampuni ya Dowercare inyozalisha bidhaa za watoto na kinamama za softcare.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla yake fupi  kuongeza mkataba wa kutangaza bidhaa hizo, ameishukuru  Kampuni hiyo kwa kumwamini tena hivyo atahakikisha kuwa bidhaa hizo zinazidi kupendwa na wateja wake na kuwavutia wengine.

Aidha amewaomba wadau na mtu mmoja mmoja kuwasaidia wanafunzi wakike wanaoshindwa kumudu gharama za kununua taulo za kike ili nao wakae kwa kujiamini na kufanya vizuri katika masomo yao.

Sambamba na hayo amesema kesho anakwenda hospitali ya Taifa Mhimbili kutoa sadaka yake kwa kutoa pempasi kwa watoto wadogo na baadhi ya wakina mama taulo za kile kwani hivyo wapenzi na mashabiki zake washirikiane nae .

“Ninamshukuru sana Mungu kwa kunipa kibali tena kuongezewa mkataba na Kampuni hii kutangaza bidhaa zake ambazo ni za uhakika na ubora mimi nimekuwa nikizitumia pia watoto wangu wakiwa wadogo wamezitumia ni Bora na salama” Amesema Zari.

No comments