SERIKALI YAGAWA MAJIKO YA GESI KWA MAMA LISHE KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
KATIKA kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi yanayotokana na hewa ya ukaa Serikali imegawa majiko 200 ya gesi kwa mama lishe na baba lishe wa masoko ya Jimbo la ilala ili waweze kutumia nishati mbadala.
Akigawa majiko ya gesi leo Agosti 18 kwa mama Lishe wa soko la Machinga Complex, Mchikichini na ilala, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu, amesema dunia kwa sasa imebadilika na kueleza Tanzania ni sehemu ya nchi ambayo imekuwa ikipambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Zungu amesema katika kujali maisha ya wafanyabiashara Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuwaunga mkono Wafanyabiashara wa mama lishe na baba lishe kwa kuwagawia majiko Ili kurahisisha mapishi yao kwa kutumia nishati mbadala badala ya kutumia kutumia kuni na mkaa.
Amesema wameamua kugawa majiko ya gesi kwa mama lishe wa Ilala ,soko la Machinga Complex ,Ilala Boma ,Mchikichini na gerezani kwa mama lishe ili kuwasaidia kupika chakula na kupasha moto kila wakati kwa wateja wao.
Naibu Spika Zungu ambaye pia ni Mbunge wa ilala amesema serikali imejipanga na inamkakati wa kupunguza vifo kwa kinamama ambavyo vimekuwa vikisababishwa na kuni pamoja na mkaa.
"Athari za kutumia kuni pamoja na mkaa ni sawa na mtu ambaye anavuta sigara 300 hivyo kupitia majiko haya maisha yenu yatabadilika pamoja na kuokoa gharama zenu ambazo mlikuwa mkitumia kwa ajili ya kununua kuni mkaa"amesema Zungu.
Aidha aliwasii waondokane na kasumba kwamba chakula ukipika na gesi sio kizuri badala yake watumie gesi katika mapishi yao ili Moshi katika chakula.
Naye Meneja Soko la Machinga Complex Stella Mgumia, ameipongeza Serikali kwa kuwaunga mkono baba lishe na mama lishe kwa kuwapatia majiko ya gesi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amesema majiko hayo yatawasaidia kuondokana na gharama za kununua mkaa na kuni kwa ajili ya kupikia chakula .
Katika hatua nyingine Meneja huyo amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo ambayo sio rasmi kuondoka na kwenda kufanya biashara zao Machinga Complex .
"Natoa rai kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wanaouza mihogo na chips pembezoni mwa barabara kuondoka mara moja nawaomba mje katika soko la machinga Comprex ambalo ni mahususi kwa ajili yenu.
Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa majiko hayo mama lishe katika soko la Machinga Comprex Hadija Rajabu ameishukuru Serikali kwa msaada wa Mitungi hiyo ambayo itaenda kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku na kuwapunguzia kero ya moshi wakati wa kupika.
Post a Comment