MKURUGENZI PURA AFUNGUKA KUHUSU MIPANGO YA GES NCHINI .
.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni akiwa Katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wafanya kazi wa PURA
Katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Mwamba wa habari.
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeelezwa kuwa itatumia Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kueleza Miradi wananchi Miradi wanayosimamia na tafiti walizofanya kwenye mafuta na gesi asilia hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Katika banda la PURA Katika Maonesho ya biashara ya 47 ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni ametaja miongoni mwa Miradi hiyo kuwa na Mradi wa kubadili gesi waliyogundua katika Bahari kuu na kuweka kwenye hali ya kimiminika.
Amesema Katika tafiti zilizoanza tangu miaka 50 iliyopita na wamegundua gesi ambayo ni chanzo cha nishati nchini na hadi sasa wamechimba visima 96 vya gesi na Kati ya hivyo 44 vilikutwa na gesi na vingine vilivyobaki havikuwa na gesi.
Ameongeaa kuwa gesi iliyopo nchini inazalishwa kutoka Songosongo, Mnazibey na Kwara na imekuwa ikitumika katika kuzalisha umeme wa viwandani, majumbani na kadhalika.
Aidha amebainisha kuwa katika tafiti zao hadi sasa wamegundua futi za ujazo Trilioni 57.5 za gesi.
Amesema kuwa kama PURA ndiyo Mamlaka ambayo inamshauri Waziri wa Nishati katika Uwekezaji wa nisahti ya mafuta na gesi katika Mkondo wa Juu.
Post a Comment