WELLWORTH HOTEL AND LADGES WATAJA KUFURAHIA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUKUZA UTALII
Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd Zulfikar Ismail akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Na Francisco Peter, Dar es Salaam.
Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges inayomiliki hoteli za Kunduchi Beach,Embassy na Mikumi Wildlife Lodge imempongeza Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri kwa kuweza kufanya mahisiano mazuri baina ya serikali na wadau wake wa maendeleo ambapo wao wawekezaji ni sehemu yake.
Hayo yamesemwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd Zulfikar Ismail ambaye amesema kampuni hiyo inamilikiwa na watanzania wazawa wenyewe kwa asilimia 100 huku wakimiliki miradi mingine kadhaa ya uwekezaji.
"Tunapenda kuwajulisha kuwa kupitia uwekezaji wetu sisi kama kundi la Wellworth tumeweza kutoa ajira kwa wafanyakazi wapatao 525 na kuchangia pia Pato la taifa kwa njia mbali mbali ," amesema Ismail.
Ismail amezitaja hoteli zake hizo kuwa inamiliki hotel ya Ngorogoro Oldean Mountain Lodge,Lake Manyara Kilimamoja Lodge,Tarangire Kuro Treetops Lodge,Ole serai Luxury Camp -Moru Kopjes,Ole serai Luxury Camp- Turner Springs,Ole serai Luxury Camp- Kogatende,Ole serai Luxury Camp- Seronera,Kunduchi Wet n Wild Waterpark.
Hoteli zingine ni Kinduchi Beach hotel,Zanzibar Beach resort, huku zilizokwenye ujenzi kwa sasa ni Serengeti Lake Magadi Lodge,Mikumi Wildlife Lodge na Zanzibar Whispering palms.
"Katika maono tuliyonayo ya kuzidi kuongeza fursa mwakani tutakuwa na hoteli 22 tumejipanga kuwekeza zaidi kwenye utalii ambapo hali ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutengeneza filamu ya Royal Tour serikali imetusaidia sana katika kupata idadi kubwa ya watalii kujanchini,"amesema Ismail.
Mkurugenzi huyo amesema wameweza kuppata "booking"za wageni hadi 2025 ambapo kwa kazi wanazofanya katika nchi upande wa utalii ni moja ya wadau wenye uaminifu.
Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Josephine Makundi amesema kwamba hotel na lodges zote za kampuni hiyo zinauwezo wa kuwahudumia wateja wanaolala zaidi ya elfu moja katika usiku mmoja.
Akizungumza juu ya Kampuni hiyo Afisa Sheria na Utawala wa Kampuni hiyo Simoni Nguka amesema kwamba
kuhusu umiliki wa Embassy Hotel Nguka amesema kwamba kampuni hiyo ilinunua jengo la Embassy Hotel kutoka kwa kampuni ya Enterprise Tanzania Limited ambaye ndie muuzaji wa jengo.
"Tulinunua jengo hili kutoka kwa muuzaji wa jengo na wala sio kutoka serikalini kwa utaratibu wa biashara ya kawaida " free buyer na free saler " na limenunuliwa baada ya kujiridhisha juu ya umiliki wake ambao haukutuonyesha uwepo wa serikali katika jengo hilo wala uwepo wao katika kampuni ya muuzaji ambao ndio waliokuwa wamiliki wa jengo kabla ya kuliuza kwetu".
Aidha amesema kwamba baada ya kununua jengo walisajili mradi wa uwekezaji kupitia kituo cha uwekezaji Nchini (TIC) nakupewa cheti cha usajili namba.031964 kilichotolewa 28/06/2013 hata hivyo tulikamilisha taratibu za kupata mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 23 kutoka katika benki mbalimbali lakini mikopo hiyo kwasasa imefutwa baada ya mradi kukumbana na changamoto mbalimbali na kushindwa kuanza kwa wakati.
"Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa kesi Mahakamani baina ya waliokua wafanyakazi wa hotel hiyo na iliyokuwa menejimenti yao( sio sisi) pia kesi baina yetu na muuzaji wa jengo kukiuka masharti ya mkataba hivyo kesi hii bado inaendelea Mahakama ya rufaa.
Amesema kwamba waliinunua kutoka serikalini mwaka 1997 ambayo ni miaka 26 kwasasa
Post a Comment