TCB BANK YATOA VIFAA VYA USAFI KATIKA SOKO LA SAMAKI FERRY KIVUKONI JIJINI DAR ES SALAAM
Na Prona mumwi
Tanzania Commercial Bank (TCB) imesema itahakikisha inashirikina na Wafanyabiashara katika nyanja mbalimbali ikiwemo kukamilisha usafi wa Mazingira mahala pao pa kazi ili kusaidia kuondokana na milipuko ya magomjwa.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam Lameck Buberwa Meneja wa Tawi la kigamboni TCB bank katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi kwa Umma Mwaka 2023 ambapo wameadhimisha kwa kukabidhi vifaa vya Usafi katika soko la Samaki Ferry Kivukoni ambapo amesema wametambua soko hilo ambalo limekuwa linatoa huduma ya chakula hivyo ni budi liwe safi muda wote kutokana kwani Msongamano wa watu kusitokee mlipuko wa magonjwa .
"tumetoa vifaa hivi vya usafi wa Mazingira leo lengo ni kusaidia soko hili Mazingira yake yanakua safi na salama kwani hii ni sehemu ya chakula hivyo tunaomba mpokee vifaa hivi huu ni mwanzo tu tutaendelea kushirikiana zaidi hata katika kukamilisha miradi kupitia huduma zetu za kibenki tunazozitoa ikiwemo kufungua akaunti utoaji mikopo ya riba nafuu"amesema Lameck
Sambamba na hayo Meneja amesisitiza uongozi huo wa soko wanahitaji kushirikiana ili kuinua vipato vyao ikiwemo kuwafungulia akauti kuwapaa semina ya matumizi ya fedha ili hata wakikopa na mikopo popote katika taasisi wasifirisike kwa kushindwa kurejesha.
Naye Afisa Afya wa Soko la Feri Mary Mkwavi ameshukuru Benki hiyo kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani suala la usafi ni la kila mtu na halikwepeki ni kila mahali mtu anapokuwa hivyo vifaa hivyo vitawasaidia kusafisha soko na kuwa na Mandhari nzuri zaidi isiishie hapo wawakumbuke mara kwa mara .
Kwa Upande wake Kaimu Mkuu wa Soko la samaki Feri Ally Kasembe amesema kuna umuhimu taasisi za kifedha kuwa karibu na Wafanyabiasha wa soko hilo kwani jambo hilo wakiwa la ukaribu itawashawishi wafanyabiashara kufungua akaunti na kuweza kukopa na kuhifadhi fedha zao kupitia benki ya TCB
Post a Comment