Ads

MADINI CHUMVI YALIYOPATIKANA WILAYA YA MANYONI KUWA CHANZO KIPYA CHA MAPATO

 


MKUU wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota akizungumzia Madini Chumvi yaliyopatikana Kata ya Majiri Kijiji cha Mpandagani wilayani humo katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jana Juni 23,2023 kuwa ni chanzo kipya cha mapato katika Halmashauri ya wilaya hiyo.

Na Dotto Mwaibale, Manyoni
MKUU wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota amesema kuwa Madini Chumvi katika Kata ya Majiri Kijiji cha Mpandagani yatakuwa chanzo cha mapato katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

DC Kemirembe ameyasema haya leo Juni 23,2023 katika kikao cha Kuwasilisha ripoti ya Utafti wa madini hayo uliofanywa na Wataalam kutoka Wizara ya Madini.

"Tunawashukuru sana kwa utafiti wenu mliofanya na kutuhakikishia kuwa madini chumvi yanayopatikana ni mazuri na yanafaa kwa kiwango kikubwa kwa matumizi ya binadamu, sisi kama wawakilishi wa Serikali tutahakikisha tunakitumia vizuri chanzo hiki cha mapato kwa manufaa ya jamii lakini pia ili kukuza mapato ya halmashauri YETU”. alisema Kemirembe.

Akiwasilisha ripoti hiyo Mjiolojia Mwandamizi, Charles Moye amethibitisha kuwa chumvi inayopatikana katika eneo hilo wilayani humo ni nzuri kwa matumizi ya binadamu na kuwa ni tofauti kabisa kwaubora na ile inayopatikana maeneo mengine.

"Manyoni mmebahatika kupata chumvi ambayo ni bora na ya viwango vya juu hivyo mnakila sababu ya kukilinda chanzo hiki kipya cha mapato katika wilayani yenu'" alisema Moye.

No comments