KIFO CHA MEMBE CHAIBUA MASWALI, DAKTARI AELEZEA KILICHOMUUA
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama Bernard Membe amefariki dunia mapema leo asubuhi katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.
Membe ambaye amehudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Chama Cha Mapinduzi kabla ya kwenda Chama Cha ACT- Walendo na kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ,kifo chake kimeibua maswali mengi na mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii
Tayari sababau za awali kuhusu kifo cha Mzee Membe aliyekuwa kipenzi cha wananchi wa Jimbo la Mtama na Mkoa wa Lindi kwa ujumla imeelezwa kuwa kimetokana na changamoto ya upumuaji ambapo alifikishwa katika hospitali hiyo na kupelekwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi(ICU) kwa matibabu lakini ilipofika saa mbili asubuhi akaaga dunia.
Akizungumza leo asubuhi Daktari wa Hospitali ya Kairuki ambako Membe alifikishwa kwa matibabu Dk.Asseri Mchomvu amesema walimpokea Membe saa 12:30 akiwa na changamoto ya upumuaji na hivyo jopo la madaktari wakaanza kumpatia matibabu lakini baadae akaaga dunia.
Ameeleza kuwa kabla kufariki Dunia jana Membe alifikishwa katika hospitali hiyo ambako alipatiwa matibabu na kuruhusiwa lakini leo alirudishwa tena baada ya kuzidiwa kwa changamoto ya upumuaji.
Dk.Mchomvu alipoulizwa changamoto ya Membe ilikuwa ni nini?Amejibu kwa kifupi kwamba alikuwa anasumbuliwa na upumuaji na ndio ambao madaktari walikuwa wakipambana kuokoa uhai wake lakini ikashindana na kufikwa na umauti.
Hata hivyo taarifa za kifo hicho zimeendelea kusambaa maeneo mbalimbali nchini na hiyo inatokana na umaarufu aliokuwa nao Membe enzi za uhai wake lakini katika mitandao ya kijamii nako kumeibuka maswali mengi kuhusi kifo chake kutokana na sababu mbalimbali (Tumezihifadhi)
Wakati huo huo tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na kifo hicho ambacho kimeacha simanzi kubwa .
Rais Samia amesema hivi"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina"
Membe ni nani?
Kwa mujibu historia fupi inaeleza kwamba
Bernard Kamilius Membe alizaliwa 9 Mei 1953 mkoani Lindi na amepata nafasi ya kusoma katika shule mbalimbali za ndani na nje ya Tamzania.
Katika harakati za kulitumikia Taifa pamoja na utumishi katika maeneo ya utumishi wa umma aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama katika Bunge la mwaka 2015 nchini. Mwaka 2016 Membe alitaka kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha (CCM) akashindwa kupata nafasi.Wakati huo CCM ilikuwa imemsimamisha Dk.John Magufuli ( hayati Magufuli).
Kitendo cha Membe kutaka kugombea urais kilimuingiza kwenye mgogoro na Chama chake na hivyo aliondoka na kujiunga na Chama cha ACT -Wazalendo ambapo katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 alijitosa na kugombea urais .
Sababu za kuondoka CCM ni baada ya mwaka 2019 Membe kuitwa mbele ya Kamati Kuu ya CCM na kuhojiwa kuhusu mashtaka ya kula njama dhidi ya Rais,hivyo akafukuzwa katika Chama.Hata hivyo baadae alirejea tena CCM na hivyo hadi umauti unamkuta alikuwa mwana CCM .
Je Membe ana ugomvi na mtu?
Katika medani za kisiasa hasa kwa nafasi ya Membe marafiki na maadui hawakosekani lakini ni ngumu kueleza kwamba Membe alikuwa a maadui maana hajawahi kuueleza umma ingawa siku miaka ya karibuni amekuwa na mgogoro na mmiliki wa gazeti la Tanzanite Cyprian Musiba na hiyo ni baada ya gazeti hilo kumuandika Membe
Gazeti hilo lilidai Membe alijaribu kumzuia Rais Magufuli asipewe nafasi ya kugombea tena mwaka 2020. Hivyo Membe aliamua kufungua kesi ya kuchafuliwa jina lake.Katika kesi hiyo alishinda na Musiba alimriwa kumlipa Membe mabilioni ya fedha.
Hivi karibuni Membe aliibuka tena na kuzungumza na vyombo vya habari akisisitiza kwamba lazima Musiba amlipe fedha zake kwani alimshampa nafasi mara kadhaa lakini alishindwa kukaa naye mezani, hivyo hawezi kumsamehe na anachotaka ni kuona hukumu ya Mahakama inatekelezwa
Nani atachukua mabilioni ya Membe yakilipwa na Musiba
Katika hili watalaamu wa Sheria watafafanua kwa kina ingawa pia inategemea kama Membe aliandika Wosia wa nani atakuwa mrithi wake au itategemea na maamuzi ya familia nani wa kusimamia suala hilo na kuhakikisha fedha hizo zinapatikana.
Wakili wa Membe afunguka
Wakati huo huo Wakili Jonathan Mdeme, aliyekuwa akimwakilisha Membe (63) kwenye kesi dhidi ya mwanahabari Cyprian Musiba, amesema deni la waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje kwa Musiba liko palepale na msimamizi wa mirathi ataendelea alipoishia.
Post a Comment