BONNAH AUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA SEKTA MICHEZO JIMBO LA SEGEREA
Na Heri Shaaban - Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa Mohamed Ally Kawaida , amesema Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya michezo Tanzania katika Jimbo la Segerea ambapo Mbunge Bonnah ameweza kuandaa mashindano ya Jimbo yalioshirikisha timu 64 Jimbo la Segerea .
Mwenyekiti wa (UVCCM) Taifa Mohamed Ally Kawaida, aliyasema hayo katika fainali ya mashindano ya Bonnah Cup, yaliyomalizika Mei 07/2023 katika Viwanja vya Tabata shule Wilayani Ilala ambapo Mabingwa wa 2023 Bonyokwa waliojizolea shilingi milioni 5000,000/= Kombe na Medani.
"Napongeza Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli ,katika sekta ya michezo ameweza kuunga mkono Juhudi za Rais Dkt ,Samia Suluhu Hassan kuandaa mashindano ya Jimbo la Segerea katika michezo mbalimbali Ikiwemo REDE ,mpira miguu ambapo ameunganisha vijana mbalimbali ,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa " alisema Ally.
Mwenyekiti Ally alipongeza timu hizo kudumisha Umoja na Mshikamano pamoja na Mbunge wa Segerea anafuata mbio za Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, alisema mashindano hayo yameshirikisha timu 64 zilizopo Jimbo la Segerea ,awali walianza hatua ya mtoano mpaka robo Fainali ,baadae zingine zikaingia nusu fainali mpaka kupatikana washindi katika Mpira miguu na rede.
Mbunge Bonnah Kamoli alisema Michezo ni ajira dhumuni la mashindano hayo kutafuta vipaji,kujenga mahusiano ,umoja na mshikamano katika Jimbo la Segerea.
Mbunge Bonnah Kamoli alikabidhi zawadi za mshindi wa kwanza ,mpaka wa tatu kwa mgeni Rasmi ambapo pesa hizo zilitolewa kwa wachezaji wa Mpira miguu ambapo BONYOKWA walikuwa champion wa mwaka 2023 wameondoka na Kitita cha Shilingi milioni 5000,000/= mshindi wa pili TABATA Kisiwani Shilingi milioni 3000,000= na mshindi wa Tabata Matumbi walijinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 2000,000/= katika mashindano ya Rede mshindi wa kwanza Buguruni alijinyakulia Shilingi laki 500,000= ya mashindano hayo na mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Mohamed Ally aliwapongeza kwa kuwaongeza Shilingi 500,000/= ambapo jumla waliondoka na milioni 1 uwanjani hapo
Mashindano ya Bonnah Cup ni endelevu yanafanyika Kila mwaka Jimbo la Segerea kwa kuzishirikisha timu za Jimbo la Segerea.
Post a Comment