TMA YAWAJENGEA UWEZO WANAHABARI KURIPOTI TAARIFA KWA USAHIHI
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka waandishi wa habari kuendelea kufatilia na kuripoti taarifa za hali ya hewa kwa usahihi jambo ambalo litasaidia kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendelea.
Akizungumza leo
tarehe 21/2/2023 Kibaha, Mkoani Pwani wakati akifungua warsha ya waandishi wa
habari kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu muelekeo wa msimu wa mvua za masika
kuanzia mwezi machi hadi Mei Mwaka huu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema kuwa mafunzo hayo
yatawasaidia wanahabari katika kufanya kazi zao kwa ufanisi.
“Warsha hii ni
muendelezo wa juhudi za kuhakikisha taarifa mbalimbali zinawafikia jamii kwa
usahihi ili kuleta tija na kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kwa kutoa
taarifa ambazo sio sahihi” amesema Dkt. Chang’a.
Dkt. Chang’a amewataka
waandishi wa habari kuendelea kuwa Mabalozi wazuri kwa umma, huku akitoa wito
kwa jamii kuendelea kufatilia taarifa za
hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ili waweze kupata
uelewa mpana.
Amefafanua kuwa katika kipindi hiki Mamlaka imekuwa ikifanya utabiri katika maeneo madogo madogo kuanzia ngazi Wilaya hasa yanayopata msimu mmoja wa mvua.
“Mnafanya kazi kubwa muhimu katika jamii, hivyo tunaomba iendelee kwa kutoa elimu na kutambua Mamlaka ya Hali ya Hewa ndiyo yenye dhamana ya kutoa taarifa zote zinazohusiana na Hali ya Hewa” amesema Dkt Chang’a
Post a Comment