Ads

TCU KUENDELEA KUIMARISHA MIFUMO YA UTHIBITI UBORA


Tume ya vyuo vikuu Tanzania imeendelea kuimarisha mifumo yake ya uthibiti ubora na mifumo ya ndani ya vyuo vikuu Ili kuhakikisha vyuo vikuu vinaendana na mwelekeo wa nchi pamoja na kuandaa na kuratibu mafunzo kwa viongozi, wahadhiri na maofisa wa vyuo vikuu vya umma na binafsi hapa nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo Katika usimamizi wa uendeshaji wa taasisi Zao.

Hayo yamesemwa na katibu mtendaji tume ya vyuo vikuu Tanzania  prof. Charles Kihampa wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za tume hiyo kwa kipindi Cha Miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Amesema kuwa Katika kuhakiki ubora tume imeimarisha mifumo yake ya ushauri na ukaguzi wa mara kwa mara wa kawaida na wa kushtukiza kwa mujibu wa Sheria na utaratibu zilizopo kwa lengo la kuhakikisha kuwa Elimu itolewayo na vyuo vikuu hapa nchini inakidhi viwango vya ubora  kikanda, kitaifa na kimataifa.

Aidha amesema kuwa nafasi za masomo Katika vyuo vya Elimu ya juu Katika program za shahada ya kwanza zimeongezeka kutoka 157,770 Mwaka 2020/2021 Hadi 172,168 Mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la nafasi 14,398 ya asilimia 9.1.

Pia kwa Mwaka 2022/2023 serikali imetenga kiasi Cha shilingi bilion 6.4 kupitia mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi ( higher Education for Economic Transformation- HEET) kwa ajili ya kuimarisha uthibiti ubora na uhuishaji wa mitaala ya vyuo vikuu ambapo zaidi ya mitaala 300 ya vyuo hivyo vinafanyiwa mapitio Ili kuhuishwa kwa kizingatia maoni ya wadau mbalimbali. 

No comments