Ads

TANESCO KUFIKIA MALENGO YA UZALISHAJI UMEME WA Megawat 5000 MWAKA 2025.

 



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa mwaka 2025 Shirika hilo litakuwa limefikia malengo ya uzalishaji wa Megawati 5000,kutokana na miradi kadhaa ambayo inachangia kuongeza uzalishaji wa umeme katika gridi ya taifa kila mwaka.


Ameyasema hayo kaimu Mkurugezi wa huduma kwa wateja wa shirika la umeme Tanzania  ( TANESCO) Martin Mwambene wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali ya shirika hilo na uelekeo wake kwa mwaka wa 2023 .


amesema kuwa kwa sasa shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 1,820,wakati mitambo iliyopo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,300 pekee. 


Pia Mwambene amesema  kuwa TANESCO kwa kutambua matatizo ya umeme yaliyopo nchini imekuja na mradi wa Gridi Imara ambapo katika bajeti ya mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake.


 Katika mradi wa Grid Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6000,mita laki 7za umeme, nguzo 380,000,ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa km 40,000, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takribani kilomita 948 na ujenzi wa vituo 14 vya kupooza umeme. 


Kaimu Mkurugenzi huyo amezungumzia pia maendeleo ya ujenzi katika Bwawa la Mwalimu NYerere kuwa upo katika asilimia  88 na zoezi la uwekaji maji limefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.

No comments