Ads

RAIS SAMIA ARUHUSU MIKUTANO YA HADHARA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameruhusu mikutano ya adhara ya Kisiasa kufanyika na kufuata kanuni na sheria pindi mikutano hiyo inapofanyika.

Ametoa ruhusu hiyo leo Januari 3,2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na viongozi wa kisiasa nchini ambapo amewataka kuacha siasa za matusi bali wakosoe pale wanapoona kuna mapungufu yamejitokeza.

Aidha amesema kumekuwa na siasa za kutukana baadhi ya viongozi walioko madarakani ambapo ni kosa na nikinyume na maadili ya nchi yetu hivyo waendelee kukosoa pale Serikali inapokuwa imekosea.

Amesema ni vizuri kwa vyama vingine kutoa mtazamo wao pale Serikali inapokuwa imejisahau ili iweze kutekeleza jambo hilo ili kuweza kuwaonesha wananchi kuwa Serikali inafanya kitu.

“Siwezi kuwaita ni wapinzani, kwamaana sioni upinzani uliopo kwenye hili maana wakikosoa kitu ambacho hakichafanywa na Serikali, tunayachukua na kuyashughulikia ili Wananchi waone Serikali iliyopo madarakani inafanya kazi”. Amesema Rais Samia.

Amesema kwenye maridhiano kati ya Chadema na CCM pamoja ya ripoti ya Kikosi Kazi masuala yaliyopendekezwa zaidi ni kuhusu kuruhusu mikutano ya kisiasa, katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

No comments