Ads

TUTAKOPA SANA TUTAJENGA SANA -RAIS DKT SAMIA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wanaosema awamu ya sita imekopa sana wasisahau kusema pia kwamba ndio awamu iliyojenga sana na kumaliza ujenzi wa reli yote.


Rais Samia amesema hayo leo Disemba 20, 2022 ikulu jijini Dar es salaam wakati wa utiaji saini mkataba wa wa ujenzi wa SGR kutoka Tabora hadi Kigoma.

Rais Samia amesema mkataba huo una thamani ya dola za marekani Bilioni 2. 21 na utatekelezwa kwa miezi 48 ambapo unatarajiwa kukamilika Disemba 2026.

Rais Samia ameongeza kuwa fedha ya ndani isingetosha kujenga reli yote kwahiyo ilibidi serikali ikope ili kukamilisha mradi huo.

Aidha Rais Samia amesema mikopo hiyo ni lazima ilipwe na kuitaka mamlaka ya kukusanya mapato yatakayosaidia kulipia mkopo huo.

No comments