Ads

WAVAMIZI WA SOKO LA WAMACHINGA COMPLEX DODOMA KUCHUKULIWA HATUA YA KISHERIA





Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Sinyamule Amewakata  wale wote ambao awana sifa za machinga wasiingie kwenye soko ilo kwani soko limejengwa KWa ajiiri ya wamachinga tu KWa yoyote atakayebainika  ameingia bila sifa za umachinga hatua za kisheria zitachukuliwa.

Pia amewataka wamachinga kuamia kwenye soko ilo KWa amani ,Uaminifu  na uhadilifu pasipo kuibiana Pamoja na kuzingatia usafi wa Mazingira.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa huyo wakati wa kusikiliza kero za wamachinga jijini dodoma kuhusu changamoto zinazowakabili wamachinga dodoma.


Sinyamule amesema Kuwa wapo ambao wamefanya maombi KWa kudanganya taarifa ili wapate nafasi ndani ya soko ilo, endapo wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa.

Aidha amewataka halmashauri ya jiji kutatua kero zote zinazojitokeza na ambazo zitajitokeza hapo baadae 

" Jiji endeleeni kutatua kero hizi na zitakazojitokeza Ili kuhakikisha wafanyabiashara wadodo wadogo wanafanya biashara KWa amani na endapo kama kutajitokeza upungufu wa vizimba watapangwa maeneo mengine"Amesema Sinyamule.


Pamoja hayo Sinyamule ametangaza rasmi tarehe 28 hadi 30 octpbar mwaka huu ndiyo siku ya kuaza kuingia wamachinga kwenye soko ilo uku akiwataka viongozi wa Halmashauri ya jiji kukaa eneo ilo  siku zote KWa ajiiri ya kusimamia zoezi ilo pamoja na kuwataka LATRA kuhakikisha kuwa kufikia tarehe 1  November daladala zinapitika njia ya soko hilo na kunakuwa na kituo cha kupitia na kushushia abiria.

Pia Sinyamule amewahakikishia Wamachinga fedha za mikopo zipo bali changamoto ya mikopo ni kuwa baadhi ya watu wanaunda vikundi vya watu watano ambapo ndani ya kundi ilo hakuna machinga hivyo ni vigumu kupata mkopo huo hivyo amewataka Wamachinga kuwa wahaminifu mwenye zoezi la kukopa na waunde vikundi  fedha za mikopo zipo.

Kwa upande wake Katibu tawala Mkoa wa dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema Kuwa kuna mifuko zaidi ya 69 inatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo pia kuna taasisi za fedha hivyo mikopo ipo kila mmoja atapata mkopo huo kwa kufata taratibu zilizopo.

No comments