Ads

TVLA IMEJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA MIFUGO.


Na. Wellu Mtaki, Dodoma.

Wakala wa maabara ya veterinari Tanzania ( TVLA ) imejipanga kutia mchango stahiki katika kuimarisha uzalishaji endelevu wa sekta ya Mifugo , usalama wa chakula Pamoja na kuchangia uchumi wa taifa kupitia utoaji wa huduma bora za uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya Mifugo kwa gharama nafuu.


Hayo yamesemwa na mtendaji mkuu wa Wakala ya maabara ya veterinari Tanzania Dkt. Stella Bitanyi wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini dodoma juu ya Taarifa ya mwenendo wa utoaji uhuduma wa Wakala ya maabara ya veterinari Tanzania.


Amesema Wakala ya maabara ya veterinari Tanzania katika utekelezaji wa kazi zake unamajukumu  ya uchunguzi na utambuzi wa wanyama, uzalishaji na usambazaji wa chanjo za Mifugo, uhakiki wa ubora wa ya vyakula vya Mifugo, usajiri, utafiti wa magonjwa ya wanyama Pamoja na ushauri.


 Pia Bitanyi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wafugaji kupima na kujua ugonjwa unaomsumbua mnyama Ili kuweza kutia tiba sahihi.


" katika kipindi cha miaka mitano Kati ya 2017/2018 - September 30, 2022 jumla ya sampuli 163,722 kutoka kwa wanyama mbalimbali zilipokelewa na kufanyiwa uchunguzi na utambuzi , magonjwa yaliyotambuliwa ni mdondo/ kideri, ndigana baridi na kali, ndui kwa kuku, homa ya nguruwe, kimeta, ugonjwa wa kutupa mimba, homa ya mapafu ya ng'ombe na mbuzi, kichaa cha mbwa Pamoja na sotoka ya mbuzi na kondoo" amesema Bitanyi


Aidha amesema kuwa matumizi ya kiholela ya dawa hasa dawa aina ya antibaiotiki huweza kuwaathiri binadamu kutokana na kula mabaki ya dawa hizo Kwenye vyakula vinavyotokana na wanyama.


" Tatizo kubwa linaloikabili dunia kwa sasa ni matumizi ya kiholela ya dawa na wafugaji wanapaswa kuzingatia ushauri unaotolewa Ili kudhibiti jambo hili na inakadiriwa kwamba kufikia mwak 2030 watu zaidi ya milioni 10 watakufa kila mwaka kutokana na dawa kushidwa kuwatibu kwani vimelea vya magonjwa vitakuwa vimejenga usugu unaotokana na matumizi holela ya dawa KWa binadamu na Mifugo" amesema Bitanyi.

Wakala ya maabara ya veterinari Tanzania ( TVLA ) ni wakala ya serikali chini ya wizara ya Mifugo na uvuvi iliyozinduliwa rasmi Julai 11, 2012, wakala hii ilitokana na kuunganishwa KWa ilivyokuwa maabara juu ya Mifugo ( CLV) , vituo vya kanda vya uchunguzi wa magonjwa ya Mifugo ( VICs) , Taasisi ya Utafiti wa Ndorobo  (TTRI) Tanga pamoja na kituo cha Utafiti wa Ndorobo ( TTRC) kigoma.

No comments