Ads

TANZANIA HAITAKUWA NA UHABA WA SUKARI TENA

 



Bodi ya sukari Tanzania imeihakikishia Nchi haitakuwa na uhaba wa sukari katika kipindi cha Mwaka 2025/2026 ambapo uzalishaji utaongezeka kutoka Tani laki 380 za Sasa hadi kufikia Tani laki 756. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof.Keneth Bengesi,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023. ameeleza kuwa Serikali imekuwa inatumia zaidi ya Dolla Million 150 ambazo ni zaidi ya Sh.Billion 300 ya fedha za Kitanzania kuagiza sukari toka nje ya nchi kila Mwaka ambapo huagiza Tani laki 645 za Sukari ya matumizi ya kawaida na matumizi ya Viwandani. Kutoka na hilo amesema kuwa Uhaba huo wa Sukari utaisha katika kipindi hicho kutokana na Mikakati mbalimbali iliyojiwekea katika kuongeza uzalishaji wa Sukari Nchini. Prof Bengesi amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia suluhu hassan imedhamiria kuongeza uzalishaji wa sukari nchini kwa kujenga viwanda vingi ili kuongeza ajira kwa watanzania pia. “Serikali ya Awamu ya Sita imeweka msukumo mkubwa na mazingira mazuri katika kuhakikisha tunaelekea kuzalisha sukari ya matumizi ya viwanda, tayari kuna wawekezaji wameshaanza kuonesha nia kwenye eneo hilo. Kwa takwimu zinazoishia Juni, 2022, mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida tuliyotumia kwa mwaka mzima ni tani 440,000 na sukari ya matumizi ya viwanda tuliyoagiza kutoka nje ni tani 205,000,” amesema Bengesi. Pamoja na hayo amesema kuwa watahakikisha kuwa miradi mipya ambayo ni Kiwanda cha Sukari Bagamoyo kimeshaanza na kwa msimu huu watazalisha tani 20,000 na mwaka 2023 wanatarajia kufikia tani 35,000 ambao ndio uwezo wa kiwanda kwa sasa. “Uwekezaji wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero ni zaidi ya Shilingi bilioni 500 ambapo Serikali ina asilimia 25 ya hisa katika Kiwanda hicho. Kiwanda cha Sukari cha Kagera kuna upanuzi mkubwa sana umefanyika ambapo kwa sasa kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 140,000, ifikapo 2025/26 kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 170,000,” amesema Prof Bengesi. Hata hivyo Prof Bengesi amesema Kiwanda cha Sukari Mtibwa kinatarajia kuongeza uzalishaji kutoka tani 48,000 za sasa hadi tani 100,000 ifikapo mwaka 2025/26,na kuongeza kuwa TPC kwa sasa inazalisha tani 100,008 na wana uwezo wa kufikia tani 120,000,huku kiwanda cha Manyara kinazalisha tani 8,000 kwa sasa na kinatarajiwa kuzalisha tani 10,000 kwa mwaka 2025/26. “Miaka ya nyuma tulikuwa tunaagiza sukari mpaka tani 183,000 lakini Serikali imefanya juhudi ambapo kwa sasa tumepunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi kutoka tani 144,000 mwaka 2017 hadi tani 50,000 kufikia Juni, 2022” Amesema Prof. Bengesi. Akielezea mchango wa tasnia ya sukari katika uchumi na jamii Prof Bengesi amesema kwamba, Tasnia ya sukari inachangia zaidi ya asilimia moja ya Pato la Taifa na imeweza kutengeneza ajira za moja kwa moja zaidi ya 24,000 na zisizokuwa za moja kwa moja zaidi ya 180,00. Ameongeza kuwa katika maeneo yenye mashamba na viwanda vya sukari, huduma mbalimbali za kijamii zinatolewa, ambazo ni kwa ajili ya wafanyakazi na jamii inayozunguka mradi zikiwemo za shule na hospitali. “Patoghafi linaloenda kwa wakulima wa miwa limeongezeka kutoka Shilingi bilioni 35.4 mwaka 2010/11 mpaka bilioni 94.7 mwaka 2021/22” Amesema Prof Bengesi. Akielezea mikakati ya kuhakikisha nchi inaondokana na tatizo la upungufu wa sukari,amesema Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji wa sukari kupitia viwanda vilivyopo, ikiwemo kufanya upanuzi wa viwanda ili kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 380,000 hadi tani 671,000 katika kipindi cha miaka miwili ijayo. “Tunahakikisha kuwa miradi mipya ambayo ni Kiwanda cha Sukari Bagamoyo kimeshaanza na kwa msimu huu watazalisha tani 20,000 na mwaka 2023 wanatarajia kufikia tani 35,000 ambao ndio uwezo wa kiwanda kwa sasa. Kwa upande wa Kiwanda cha Mkulazi Morogoro wanaoanza uzalishaji wa sukari mwaka 2023, wanatarajia kuzalisha mpaka tani 50,000 ifikapo mwaka 2025/26.

No comments