TANTRADE YAUNGANISHA WAFANYABIASHARA TANZANIA NA INDIA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini Tanzania (TANTRADE) imeunganisha Kundi la Wafanyabiashara 15 kutoka India pamoja na Wafanyabiashara Tanzania kutoka Zaidi ya Sekta 10 kwa lengo la Kukuza Soko la Bidhaa za ndani kwenye Soko la Kimataifa.
Kundi hilo la Wafanyabishara hao wamekutana kupitia mkutano maalumu ulioratibiwa Tantrade kwa Ushirikiano wa ITTC, ambapo licha ya kukuza Soko la Ndani pia walifanya mazungumzo ya ana kwa ana (B2B).
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa Khamis akizungumza mara baada ya mkutano huo, amesema zitaibuliwa Fursa mbalimbali za Uwekezaji na Biashara ambapo TanTrade itatoa tathimini ya mafanikio ya mkutano huo.
"Tunaamini kwamba baada ya hapa kuna fursa ambazo zitapatikana hatimaye tutaweza kuzikusanya na kutoa tathmini yake katika siku za usoni "
Kwa upande wake kiongozi wa ujumbe huo kutoka India Dkt. Shrenk Nahar amesema wanategemea kupata bidhaa bora ambazo zitachochea mzunguko mkubwa wa kibiashara baina ya Wafanya biashara hao.
Katika mkutano huo baadhi ya kampuni zimefanya makubaliano ya awali ya kuwa na soko endelevu ikiwa ni pamoja na korosho zilizobanguliwa zaidi ya Tani 2000, Korosho ghafi tani 100 kila mwezi, Biashara ya Ngano, majadiliano ya Nano-Urea, fursa za wakala wa magari na pikipiki zinazotumia Umeme na Uendelezaji wa Miliki na Makazi

Post a Comment