Ads

WANAKAYA WAANDAE TAARIFA MAPEMA KURAISISHA ZOEZI LA SENSA.



Na. Wellu Mtaki. Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary

Senyamule amewaasa Wananchi kuandaa taarifa za kaya ili kazi ya kuhesabu watu iwe raisi na ifanyike KWa muda mfupi.

Ameyasema hayo leo 21Agost wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma. Miongoni mwa taarifa hizo ni umri wa wanakaya, hali ya ajira, Elimu, taarifa za kilimo na Mifugo, namba ya kitambulisho cha Taifa ( NIDA ) pamoja na namba za simi za wanakaya.

Pia Senyamule amewasisitiza wakuu wa wilaya wote mkoa wa dodoma KWa kushirikiana na kamati za usalama za wilaya pamoja na wakurugezi wa halmashauri kuhakikisha wanasimamia zoezi la sensa ya watu na makazi kikamilifu Kwenye wilaya zao.

Aidha amewataka wanainchi wa mkoa wa dodoma kupiga simu namba 0800110083 bule pindi kaya yoyote haitofikiwa na karani wa sensa.

" Mkoa wa dodoma tumeamua kujiongeza kuweka namba ya simu Ili kuhakikisha zoezi la sensa linafanyika kikamilifu na kila mtu anahesabiwa, mwanakaya atapiga simu na kutoa Taarifa kueleza Mtaa/ kitongoji alipo Ili kufikiwa na karani wa sensa" amesema senyamule

Senyamule amewataka makarani kuhesabu watu katika eneo alilopangiwa KWa ufasaha na kutunza siri za kaya alozohoji na kutambua kazi hiyo inafanyika KWa masilahi ya taifa katika kupanga mipango ya maendeleo.

Pia amewasihi wanainchi kuwa tayali kushiriki zoezi Ilo la sensa  23 Agost 2022 KWa faida ya watanzania wote na watambue kuwa ni kosa kisheria kukataa kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi.


No comments